Jumanne, 27 Novemba 2018

UJASIRIAMALI--JINSI YA KUPATA MTAJI BILA KUKOPA


JINSI YA KUPATA MTAJI KWAAJILI YA KUANZISHA BIASHARA BILA KUKOPA (MKOPO)
Kabla ya kujifunza kitu chochote katika makala hii, ni vyema tukajuzana kuwa, biashara haihitaji haraka kama jinsi tunavyoichukulia biashara. Biashara inahitaji utaratibu wa hatua kwa hatua, huku ukifanya tathmini kwa kila hatua (yaani unaangalia mafanikio, changamoto,  mapungufu na namna ya kutatua vizuizi vinavyojitokeza katika biashara).
Mjasiriamali mdogo anashauriwa kuanza na mtaji mdogo na kisha kuukuza mtaji huo kidogo kidogo. Ni rahisi kufikia malengo yako kibiashara endapo kama utaona kila fedha inafaa kuwa mtaji kwa kuanza biashara. Kwa mfano, umepanga kuwa, baada ya miezi mitatu (3) inatakiwa upate shilingi 1,000,000/- (Milioni moja), ili kuanzisha biashara ya kusafirisha mazao kutoka vijijini na kuyapeleka mjini, huku ukiwa na shilingi 50,000/- (elfu hamsini) mfukoni  mwako. Lakini cha kushangaza, baada ya miezi mitatu ya malengo, unajikuta una shilingi 100,000/- (Laki moja tu) ama chini ya hicho kiasi. Kwa muonekano huo, utakuwa umefeli kabisa kupata shilingi 1,000,000/- kwaajili ya kuanzisha biashara ya kusafirisha mazao mjini.
# Kosa limetokea wapi?
Kimsingi fedha ya biashara haitakiwi kukaa bila kuzungushwa na kuleta faida. Kumbe basi, ilitakiwa ile ile shilingi 50,000/- (elfu hamsini) uitazame kama mtaji unaofaa kuanzisha biashara ndogo yenye uwezo wa kukupatia hata faida ya shilingi 15,000/- (elfu kumi na tano) kwa siku. Kuna biashara nyingi za kuweza kukupatia hicho kiasi cha pesa kwa siku endapo kama utakuwa tayari kufanya kazi kwa bidii na kujituma. Kwa mfano, unaweza ukaenda soko kuu lolote lililo karibu, kisha ukanunua matunda ya shilingi 50,000/- kwa bei ya jumla na kisha ukayauza kwa  wanaojua nini maana ya matunda, ungeweza kupata faida ya shilingi 20,000/- kwa siku Hii ingekujengea msingi na mwanzo mzuri katika safari yako ya kuitafuta shilingi 1,000,000/- kama mtaji wa kuanzisha biashara ya kusafirisha mazao kutoka vijijini na kuyapeleka mjini. Hii inawezekanaje? Tuangalie hesabu ndogo hapa chini.
Kwa masoko makubwa yaliyomengi nchini Tanzania, bei za jumla za matunda ni kama ifuatavyo;-
*      Chungwa  1= shilingi 100/=, na unaweza kuuza kwa bei ya machungwa 6 = shilingi 1,000/=
*      Maembe  3 (ya ukubwa wa wastani ya kati) = shilingi 500/=, na unaweza kuuza kwa bei ya shilingi 1,000/= (elfu moja, kwa fungu la maembe 3)
*      Tikiti maji 1 (la saizi ya kati) 2,000/= hadi 3,000/=, na ukaweza kuuza kwa bei ya shilingi 4,000/= hadi 5000/= (Isipokuwa kwa mikoa ya Dae-es-Salaam, Arusha, na Pwani) kwa upande wa Tanzania,
*      Parachichi 3 (za ukubwa wa wastani ya kati) = shilingi 500/=, na unaweza kuuza kwa bei ya shilingi 500/= kwa kila parachichi 1, au kwa bei ya shilingi 1,000/= kwa fungu la parachichi 3.
Je, hii siyo faida? Na pia, ngoja nikupe siri hii msomaji wangu! Hakuna biashara iliyonzuri kama biashara inayokupatia faida inayolingana na mtaji, au faida inayozidi mtaji uliowekeza, haijalishi ni kiasi gani cha mtaji ulichowekeza. Katika biashara, unapoongeza wateja wapya, ndivyo unavyoongeza faida zaidi na zaidi.
Kwa mchanganuo huu, nategemea kutosikia neno “sina mtaji” kwa msomaji wangu aliyesoma makala hii, kwani naamini kabisa kuwa, hakuna mtu ambaye anaweza kukosa shilingi 500/= ya kuanzisha biashara ya kuuza matunda kwa watu wanaojua umuhimu wa matunda.
Mtu anawezakuwa na uwezo wa kukusanya faida ya shilingi 50,000/= (elfu hamsini) kama faida ya siku moja, lakini asiwe na maendeleo yoyote. Donald  J.Trump, na Robert  T. Kiyosaki, katika kitabu chao kinachojulikana kama “Why We Want You To Be Rich” katika masuala ya maendeleo kibiashara, walisema “Tatizo siyo kwamba tunaingiza shilingi ngapi, bali tatizon ni, tunatunza shilingi ngapi? Lakini pia wote kwa pamoja wanakubaliana kuwa, katika biashara, kwa waliowengi, “Tatizo siyo mtaji! Ila tatizo ni kukosa elimu ya biashara na ujasiriamali” nukuu za waandishi hawa zinadhihirisha ukweli kabisa kuwa, hata shilingi 1,000/= (elfu moja) ni mtaji tosha wa kuanziasha baadhi ya biashara, ila shida kubwa ni kuifanya hiyo shilingi 1,000/= izae na kuleta mtaji mkubwa zaidi.

# ANGALIZO KWA MJASILIAMALI MDOGO (MUUZAJI WA MATUNDA)
Ø  Kama una mtaji mdogo, chonde chonde usifanye biashara ya kusafiri umbali mrefu, bali fanya biashara ya kusafiri kwa umbali usiozidi lisaa limoja. Hii itakurahisishia kuwa na uhakika wa kurudia bidhaa muda wowote utakapomaliza bidhaa, na hivyo kufanya mzunguko wako kwenda haraka,  wenye tija na wenye kukupatia faida zaidi.
Ø  Usikopeshe zaidi ya nusu ya mtaji wako, maana kwa kufanya hivyo, unaweza ukajikuta unakosa fedha ya kwenda kuchukulia mzigo, wakati ukiwa umeshauza mzigo wote (ila kwa mkopo).
Ø  Mkopeshe mteja ambaye una uhakika wa kulipwa ndani ya masaa kadhaa, na siyo siku kadhaa.
Ø  Uwe mwaminifu na mkweli katika biashara zako
Ø  Itetee vyema biashara yako
Ø  Ipende biashara yako, kwa kuiona kama ndiyo kazi yako uliyoajiriwa.
Ø  Uwe na lugha nzuri kwa wateja wako! hata kama hutaki kumkopesha, si vyema ukamwambia kuwa “sikopeshi” badala yake mwambie “kwa kweli leo sina hela ya kwenda kuchukulia mzigo, mzigo huu ndio ninaoutegemea kuongezea mtaji wa leo” mteja huwa ni mwelewa sana endapo kama utatumia lugha ya kumwelewesha kwa utaratibu na bila kuharibu furaha yake aliyonayo siku hiyo.
Ø  Kuwa na bei rafiki na isiyomuumiza mteja (yaani unakuwa na watja wa kila aina, wapo wale wenye uwezo mzuri, pia wapo ambao uwezo wao ni mdogo, ila kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao,inawabidi wapate bidhaa zao ili maisha yaende) kwa mfano, kwa mjasiriamali anayeuza matunda, atakutana na wateja kama vile wagonjwa, wajawazito na wamama waliojifungua siku si nyingi. Hawa wote wanahitaji huduma ya matunda, hivyo ni vyema kwa muuzaji kujua saikolojia na uwezo wa wateja wake.

Nakushukuru kwa kufuatilia makala zangu katika blog yangu na katika kurasa zangu za mitandao ya kijamii. Usikose kufuatilia makala zangu zingine, ni rahisi sana, ingia kwenye blog yangu kisha bofya kitufe  follow  by e-mail. Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kupata makala zangu mpya.

REJEA
Trump, D.J & Kiyosaki, R.T (2006) Why We Want You To Be Reach. Rich Press
                        Publishers.New York.

Jumanne, 13 Novemba 2018

FASIHI - Uchambuzi wa maana ya Fasihi kwa mujibu wa K.W Wamitila


MAANA YA FASIHI KWA MUJIBU WA K.W WAMITILA

Wataalamu wengi wa fasihi wametoa maana ya neon fasihi kulingana na mitazamo yao,ubunifu wao, falsafa zao na hata uzoefu wao katika uwanja wa fasihi. Makala hii, imeangazia zaidi katika kuichambua maana ya fasihi iliyotolewa na mwana fasihi Kyallo Wadi Wamitila katika kitabu chake cha Kamusi Ya Fasihi; Istilahi na Nadharia, kilichochapishwa mwaka  2003.

Maana ya Fasihi kwa mujibu wa Wamitila (2003)
“Fasihi ni kazi za kisanaa au zilizotumia lugha kwa usanii na zinazowasilisha suala fulani pamoja kwa njia inayoathiri, kugusa na huacha athari fulani na uonyesha ubunilizi na ubunifu fulani na zinazomhusu binadamu”

Fasihi ni kazi ya Kisanaa na yenye kutumia lugha
Hii ina maana kuwa, fasihi ni sanaa kama zilivyo sanaa zingine kama vile muziki, uchoraji, ususi, ufinyanzi n.k, isipokuwa fasihi inatumia lugha ili kufikisha ujumbe wake, tofauti na matawi mengine ya sanaa.

Fasihi ni kazi inayowasilisha suala fulani pamoja
Fasihi ni lazima iwe na mada, jambo au tukio mahususi ambalo inawasilisha, na jambo hilo ni lazima liwasilishwe kwa pamoja. Hii ina maana kuwa, kama jambo au kisa ni lazima kiwasilishwe chote kwa mtiririko unaofaa na uwe ndani ya kazi moja.

Iwasilishwe kwa njia inayoathiri na kugusa
Lengo la msanii ni kuufikisha ujumbe katika jamii kama jinsi yeye anavyohitaji ufike au zaidi yahata ambavyo yeye anahitaji ufike. Ili lengo hilo lifanikiwe, ni lazima kutumia njia zenye kuweza kumgusa msomaji na kuikonga vyema nafsi na moyo wake kwa kile msanii alichokiwasilisha. Kwa mfano, msanii anahitaji kuwasilisha ujumbe juu ya unyanyasaji unaofanywa na baadhi ya viongozi katika nchi, itambidi msanii atumie sauti za hudhuni zilizojaa manyanyaso na uteswaji uliokithiri

Fasihi huacha athari
Kutokana na uhalisia wa fasihi katika jamii nyingi, basi kazi ya fasihi huweza kusababisha matokeo yoyote kutokea katika jamii. Hii ina maanisha kuwa ujumbe umefika mahali ulipotakiwa kufika na ndiyo maana ukasababisha matokeo kutokea.

Ubunilizi na ubunifu
Ubunilizi na ubunifu ni vipengele muhimu sana katika kazi yoyote ile ya fasihi. Fasihi bila ubunifu ni sawa na makala, kama zilivyo makala zingine. Ni vigumu kujihakikishia usalama kwa msanii wa fasihi pasipo kutumia ubunifu. Tukumbuke kuwa, katika jamii kuna makundi ya aina nyingi, hivyo lazima kazi ya fasihi iibue ukinzani endapo kama unakosoa matabaka yenye nguvu.

Zinazomhusu binadamu
Fasihi ni zao la jamii, hivyo ni vyema kazi za fasihi zimhusu zaidi binadamu kwani ndiye mwenye utashi na akiri yenye uwezo wa kufikiri. Hii haina maana kuwa wahusika wanyama hawahitajiki, lahasha! Kinachozungumziwa hapa ni ujumbe umuhusu binadamu.


Marejeo
Wamitila K.W (2003) Kamusi ya Kiswahili; Istilahi naNadharia.Focus
                   Publication.Nairobi.



Jumatano, 8 Agosti 2018

Find Japanese Used Cars?

 Find Japanese Used Cars?

<a href="https://tracking.niji7.com/tracking?t=ddf6aa760248ccd61f8a95681299daf740cf2f30446e0f8a757b73f6bf8ab2dd&ap_id=929&eco_id=1&link_id=1" class="niji7-affiliate" title="Japanese Used Cars | BE FORWARD"><span class="niji7-affiliate-text">Find Japanese Used Cars?</span></a>

<a href="https://tracking.niji7.com/tracking?t=ddf6aa760248ccd61f8a95681299daf740cf2f30446e0f8a757b73f6bf8ab2dd&ap_id=929&eco_id=1&link_id=1" class="niji7-affiliate" alt="Japanese Used Cars | BE FORWARD"><img src="https://tracking-cdn.niji7.com/img/beforward_logo_120x90.jpg" class="niji7-affiliate-img" width="120" height="90"></a>

<a href="https://tracking.niji7.com/tracking?t=ddf6aa760248ccd61f8a95681299daf740cf2f30446e0f8a757b73f6bf8ab2dd&ap_id=929&eco_id=1&link_id=1" class="niji7-affiliate" alt="Japanese Used Cars | BE FORWARD"><img src="https://tracking-cdn.niji7.com/img/beforward_logo_300x250.jpg" class="niji7-affiliate-img" width="300" height="250"></a>

<a href="https://tracking.niji7.com/tracking?t=ddf6aa760248ccd61f8a95681299daf740cf2f30446e0f8a757b73f6bf8ab2dd&ap_id=929&eco_id=1&link_id=1" class="niji7-affiliate" alt="Japanese Used Cars | BE FORWARD"><img src="https://tracking-cdn.niji7.com/img/beforward_logo_468x60.jpg" class="niji7-affiliate-img" width="468" height="60"></a>

<a href="https://tracking.niji7.com/tracking?t=ddf6aa760248ccd61f8a95681299daf740cf2f30446e0f8a757b73f6bf8ab2dd&ap_id=929&eco_id=1&link_id=1" class="niji7-affiliate" alt="Japanese Used Cars | BE FORWARD"><img src="https://tracking-cdn.niji7.com/img/beforward_logo_728x90.jpg" class="niji7-affiliate-img" width="728" height="90"></a>

Jumamosi, 14 Julai 2018

FASIHI LINGANISHI---Mchango wa Tafsiri katika Fasihi ya Kiswahili


CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ASKOFU MKUU YAKOBO
                                                                                              
KITIVO CHA SANAA NA SAYANSI ZA JAMII
IDARA YA LUGHA, ISIMU NA FASIHI
 JINA LA KOZI:                     FASIHI LINGANISHI YA KISWAHILI
 MSIMBO WA KOZI:           SW 338
 JINA LA MHADHIRI:         MIGODELA, W.
 AINA YA KAZI:                   KAZI YA KIKUNDI
 KUNDI NAMBA:                 2
 WASHIRIKI
S/N.
               JINA
NAMBA YA USAJILI
SAHIHI
01.
CYPRIAN SIMEO, S
45289

02.
KANANI EUGENIA
45325

03
KWILASA DANIEL
45343

04.
MWAIPONJ A ANNE
45387

05.
MWAKYANDO SAMWEL
45391

06.
PONERA JESKA, L
45428

07.
TAMIMU RAJABU, A.
45447

08.
MUNG’ONG’O WITNESS
45466

09.
MBIJIMA VICTOR
45506

SWALI;
Mchango wa Tafsiri katika Fasihi ya Kiswahili.


Utangulizi
Dhana ya Tafsiri na Fasihi Linganishi kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali.
Mwansoko na wenzake (2006) wanafasili Tafsiri kuwa ni zoezi la uhawilishaji wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja hadi nyingine.
As-safi akimnukuu Dubois (1974) anaeleza kuwa Tafsiri ni uelezaji katika lugha nyingine au lugha lengwa wa kile kilichoelezwa katika lugha nyingine (lugha chanzi) ikihifadhi maana na mtindo wa matini chanzi.
Catford (1965:20) anasema tafsiri ni kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi kutoka lugha moja (lugha chanzi) na kuweka badala yake mawazo yanayolingana katika lugha nyingine (lugha lengwa).
Boldor (2003) akimrejelea Compbell (1926) Fasihi Linganishi ni taaluma inayochunguza uhusianao uliopo baina ya fasihi mbili au zaidi nje ya mipaka ya kitaifa kwa njia ya kulinganisha mfanano na msigano
Henry Remak (1971) anafasili Fasihi Linganishi kama uwanja wa kifasihi unaohusika na uchunguzi na mahusianao ya kifasihi nje ya mipaka ya nchi moja, pia kati ya fasihi na fani nyinginezo. Kwa maelezo haya ya Remak tunachoweza kusema ni kwamba Fasihi Linganishi haiishii kuangalia mahusino ya kifasihi peke yake bali huangalia mahusiano kati ya fasihi na fani nyinginezo zisizo za kifasihi.
Wamitila (2003) anaeleza kuwa fasihi linganishi  inahusu uchambuzi wa maandishi ya wakati mmoja na aina moja na katika lugha mbalimbali kwa  nia ya kumiliki sifa zinazoyahusisha  kama athari, vyanzo, sifa zinazofanana na tofauti za kiutamaduni. Anaendelea kueleza kuwa inawezekana kufanya hivi kwa nia ya kuangalia matapo mbalimbali, maendeleo au hata nadharia za kiuhakiki. Fasihi ya namna hii iliweka misingi na juhudi za wanaisimu kuanza kuilinganisha lugha mbalimbali katika karne ya kumi na tisa.
Kutokana na fasili zote hizo kuhusu tafsiri tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa, tafsiri ni uhawilishaji wa mawazo, ujumbe au taarifa iliyopo katika maandishi kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa bila kupoteza maana ya msingi na mtindo uliotumika katika matini chanzi. Na maana katika tafsiri inatakiwa iendane na lengo la mtunzi wa matini chanzi lakini pia kwa kuzingatia utamaduni wa jamii unayoitafsiriya.
Pia Fasihi Linganishi ni aina ya fasihi ambayo inajikita zaidi kutumia mbinu za kiulinganishi baina ya kazi mbili za kifasihi ili kujua sifa fulani fulani kama vile kufanana kwa kazi hizo, tofauti za kiutamaduni katika kazi hizo, kujua ulinganishi katika lugha yaani sarufi ya lugha katika kazi hizo za kifasihi.
Historia na Maendeleo ya Tafsiri nchini Tanzania.
Wanjala (2011) anaeleza kuwa, historia ya tafsiri imeangaliwa kwa kuegemea vipindi muhimu vya maendeleo na mabadiliko ya elimu na utamaduni. Nchini Tanzania, tafsiri haina historia ndefu sana kwani imeanzia mnamo karne ya 19 na inaweza kugaiwa katika vipindi vitatu vikuu navyo ni kabla ya utawala wa kikoloni, wakati wa utawala wa kikoloni na baada ya uhuru.
Kabla ya utawala wa kikoloni
Kabla ya utawala wa kikoloni wamishionari walitafsiri vitabu mbalimbali vya kikristo ikiwemo Biblia Takatifu kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili na lugha nyingine za makabila kwa lengo la kueneza dini na ustaarabu wa kikristo kwa waafrika.

Kipindi cha Ukoloni
Hiki ni kipindi kuanzia miaka ya 1800, katika kipindi hiki, wakoloni hasa waingereza walitafsiri maandiko mbalimbali ya kitaaluma na fasihi ya Ulaya kwa lugha ya Kiswahili. Vile vile kabla ya uhuru zipo baadhi ya kazi za fasihi zilizotafsiriwa na watanzania. Kwa mfano tamthiliya ya MZIMU WA WATU WA KALE iliyotafsiriwa na Mohammed Said Abdalla (1960) kutoka lugha ya kiingereza Shrine of The Ancestors.
Baada ya Uhuru
Baada ya uhuru ambapo ni kuanzia mwaka 1961. Katika kipindi hiki wapo wataalamu waliofanya juhudi za kutafsiri vitabu mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili. Mfano mzuri ni Mwalimu Julius K. Nyerere ambaye alitafsiri vitabu viwili vya mwandishi mashuhuri wa Tamthiliya wa huko Uingereza aitwaye William Shakespeare ambavyo ni tamthiliya ya JULIUS KAIZARI (Julius Caesar, 1963) na tamthiliya ya MABEPARI WA VENIS (The Merchant of Venis, 1969). Kazi nyingine zilizotafsiriwa baada ya uhuru ni WIMBO WA LAWINO (Song of Lawino) iliyotafsiriwa na Paul Sozigwa (1975), riwaya ya UHURU WA WATUMWA (The Freeing of the Slaves in East Africa) iliyotafsiriwa na East African Literature Bureau (1967), NITAOLEWA NIKIPENDA (I Will Marry When I Want) iliyotafsiriwa na Crement M. Kabugi (1982).
Kwa ujumla maendeleo ya taaluma ya tafsiri nchini Tanzania yamepiga hatua kubwa kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia. Taaluma ya tafsiri inafundishwa katika elimu ya sekondari na katika vyuo vikuu mbalimbali. Pia taasisi na asasi zinazojishughulisha na tafsiri zimeongezeka kwa mfano Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA), Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI) na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).

Mchango wa Tafsri katika Fasihi ya Kiswahili.
Tafsiri imesaidia katika kueneza dini na vipengele vingine vya utamaduni kutoka mataifa ya nje. Tafsiri ni nyenzo ya kuenezea utamaduni kutoka taifa moja kwenda jengine au kutoka jamii moja kwenda nyingine. Kwa mfano kutokana na Wazungu kutafsiri Biblia na Waarabu kutafsiri Kur-An kwa lugha ya Kiswahili, kulisababisha waafrika kwa ujumla kubadilisha dini zao za kijadi na kufuata dini ya Ukristo na Uislamu.
Tafsiri imesaidia katika kukuza lugha na fasihi ya Kiswahili. Lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa vipengele muhimu sana katika utamaduni wa Tanzania kwa sababu Kiswahili ni lugha rasmi, lugha ya taifa na Tunu ya taifa. Kabla ya kuwepo taaluma ya Tafsiri, lugha ya Kiswahili ilionekana kudumaa hasa katika nyanja ya sayansi na teknolojia. Lakini baada ya kuwepo taaluma hii, wataalamu na Taasisi mbalimbali za Kiswahili zimekuwa zikifanya jitihada za kutafsiri vitabu vya lugha mbalimbali kwenda lugha ya Kiswahili pamoja na kutafuta Istilahi na Misamiati ya Kiswahili inayoweza kwenda sambamba na Istilahi za Kisayansi. Mfano wa istilahi hizo ni kama vile Password – Nywila, Keyboard – Kicharazio, Scanner – Mdaki, Flash Disc – Diski Mweko na Mouse – Kiteuzi.
Tafsiri ilisaidia kuongeza hamasa ya usomaji wa kazi za kifasihi. Historia inaeleza kuwa, wakati wa ukoloni fasihi ilidumaa kwa sababu Waafrika hawakuwa na mwamko wa kusoma vitabu na kazi nyingi za kifasihi ziliandikwa kwa lugha ya Kiingereza kwa lengo la kuwafurahisha Mabwana. Lakini baada ya wataalamu wa fasihi kuanza kutafsiri kazi mbalimbali za fasihi ya Ulaya kwa lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za makabila mwamko wa kusoma vitabu uliongezeka. Mfano wa vitabu vya fasihi vilivyotafsiriwa wakati wa ukoloni ni MZIMU WA WATU WA KALE (Shrine of the Ancestors) iliyotafsiriwa na Mohammed Said Abdalla (1960). Pia kuna kazi mbalimbali za kifasihi zilizotafsiriwa baada ya uhuru, miongoni mwao ni Juliasi Kaizari (Julius Caesar) (1963) na MABEPARI WA VENIS (The Merchant of Venis) (1967), zote hizo zimetafsiriwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Baada ya hapo kazi mbalimbali za kifasihi kama vile hadithi fupi, Riwaya, Tamthilia na Mashairi yalitafsiriwa kutoka lugha mbalimbali kwenda katika lugha Kiswahili. Vile vile kazi za fasihi ya Tanzania zilitungwa na kupelekea kukua na kuenea fasihi ya Kiswahili.
Tafsiri imesaidia katika kukuza elimu nchini Tanzania. Elimu ikiwa ni sehemu ya utamaduni wa Tanzania, imepiga hatua kutokana na maendeleo ya mitaala na mbinu mbalimbali za kufundishia. Tafsiri ni miongoni mwa mbinu inayotumiwa na walimu wengi ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafikia lengo la kujifunza kwa mujibu wa viwango vyao. Juhudi mbalimbali zinachukuliwa katika kukuza elimu ya Tanzania. Miongoni mwa juhudi hizo ni kutafsiriwa kwa vitabu vya masomo mbalimbali ili visaidie katika marejeleo. Vile vile taaluma ya tafsiri imekuwa ni kozi muhimu katika shule za sekondari na vyuoni ili kuwapa wanafunzi uwezo wa kuitumia taaluma hii ili waweze kujiajiri kwa kutafsiri kazi mbalimbali.
Tafsiri imesaidia katika kuibua nadharia mpya ya Fasihi Linganishi. Kama ijulikanavyo kuwa fasihi ni sanaa na sanaa ni sehemu ya utamaduni. Kwa mujibu wa kitabu cha “Utangulizi wa Nadharia ya Fasihi Linganishi” kilichoandikwa na Athumani S. Ponera (2014) ni kwamba, lengo la nadharia hii ni kuchunguza kufanana na kutofautiana kati ya fasihi ya Tanzania na fasihi ya mataifa mengine hasa Amerika na Ulaya na hata kazi za mwandishi mmoja na mwandishi mwingine au kazi tofauti za mwandishi mmoja hususani katika vipengele mbalimbali vya utamaduni pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Kwa hiyo kutokana na maelezo hayo ni wazi kuwa kuwepo kwa kazi nyingi za mataifa ya nje zilizofasiriwa kwa lugha ya Kiswahili na zile ambazo hazijafasiriwa ni sababu tosha iliyomsukuma mwandishi kuanzisha mjadala huu wa nadharia mpya ya fasihi linganishi kama ilivyo kwa nadharia ya isimu linganishi.
Tafsiri imesaidia katika kukuza biashara na kuinua uchumi wa Taifa. Kama tulivyotangulia kusema kuwa, utamaduni ni utu na utu ni muhimu katika maisha ya watu. Biashara ni miongoni mwa sekta inayounganisha watu wa aina tofauti.  Kuwepo kwa utu katika biashara ndio kutasaidia kukuza biashara na uchumi wa nchi yetu. Mchango wa tafsiri katika biashara ni kuwa mikataba mingi ya biashara na uwekezaji nchini Tanzania inatafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi kupata haki zao. Vile vile matangazo mbalimbali ya kibiashara na taarifa nyingine katika vyombo vya habari kama vile magazeti hutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili kila mwananchi apate kufaidika na huduma zinazotolewa.
Tafsiri imesaidia kuingiza utanzu mpya wa Fasihi Andishi katika fasihi ya Kiswahili. Hapo mwanzo kabla ya tafsri, Fasihi ya Kiswahili haikuwa na utanzu wa Tamthiliya lakini kwa kutumia tafsiri hivi sasa Tamthiliya ni moja kati ya tanzu muhimu katika Fasihi ya Kiswahili. Mifano ya Tamthiliya zilizo tafsiriwa ni pamoja na tamthiliya ya JULIUS KAIZARI (Julius Caesar, 1963) na tamthiliya ya MABEPARI WA VENIS (The Merchant of Venis, 1969), WIMBO WA LAWINO (Song of Lawino) iliyotafsiriwa na Paul Sozigwa (1975), NITAOLEWA NIKIPENDA (I Will Marry When I Want) iliyotafsiriwa na Crement M. Kabugi (1982).
Vilevile tafsiri imesaidia kueneza Fasihi ya Kiswahili na utamaduni wake, kuna kazi za fasihi ya Kiswahili zilizotafsiriwa kwa lugha nyingine za kigeni kwa mfano Riwaya ya Utengano imetafsiriwa kama Separazione katika lugha ya Kiitaliano, hii inaashiria kuwa fasihi ya Kiswahili imeenea hadi mataifa mengine.





Mchango wa Tafsiri katika Fasihi Linganishi ya Kiswahili
Mbali na mchango wa Tafsiri katika Fasihi ya Kiswahili lakini pia Tafsiri imekuwa na mchango mkubwa sana katika Fasihi Linganishi ya Kiswahili, miongoni mwa mchango wa Tafsiri katika Fasihi Linganishi ya Kiswahili ni pamoja na:
Tafsiri hutusaidia kujua na kuliganisha tamaduni za jamii nyingine na ile iliyoandikiwa tafsiri. Kwa mfano katika Tamthilia ya NITAOLEWA NIKIPENDA (I Will Marry When I Want) iliyo andikwa na Ngugi Wa Thiong’o na kutafsiriwa na Crement M. Kabugi (1982). Tamthilia hii imetungwa katika mazingira ya jamii ya Kikuyu, hivyo Tafsiri ya tamthilia hii imesaidia kujua utamaduni wa Wakikuyu. Kwa mfano katika ukurasa wa 65, tunaweza kuona jinsi ndoa ya Kikuyu inavyofungwa, utaratibu wa utoaji mahari pamoja na nyimbo ziimbwazo wakati wa sherehe.
Pia kupitia Tafsiri tunaweza kujua historia ya jamii husika. Katika Tafsiri ya Tamthilia ya NITAOLEWA NIKIPENDA tunaona historia ya Taifa la Kenya tangu wakati wa ukoloni hadi wakati wa Uhuru. Kwa hiyo hapa tunaelewa yale yote wananchi wa Kenya waliyoyapitia wakati wa Ukoloni, kwa mfano katika uk. 32 mwandishi anaonesha adha walizopitia wananchi wa Kenya katika harakati za kupigania uhuru na baadae wakafanikiwa, uk 33. Pia tunaona katika uk. 34 wananchi wanaingia katika kipindi kingine cha uhuru lakini bado wanaendelea kupata adha zilezile kama walizozipata wakati wa Ukoloni.
Tafsiri husaidia kukuza Fasihi ya lugha lengwa. Kupitia Tafsiri, Fasihi ya lugha lengwa inanufaika na kuingizwa vipengele kadhaa vya lugha hususani misemo au methali ambazo hazikuwepo katika lugha lengwa, hivyo kwa kutafsiri misemo hii lugha lengwa nayo pia itakuwa imenufaika na misemo hiyo. Kwa mfano, msemo; “when axes are kept in a one basket they must necessarily knock agaist each other” umefasiriwa kama;“vyuma vikiwa katika gunia moja havikosi kugongana” uk. 24. Kwa hiyo tunaweza kuwa tumeongeza msemo mwingine katika Kiswahili kupitia Tafsiri hii.
Vilevile tafsiri imeongeza idadi ya machapisho ya vitabu vya Fasihi ya Kiswahili na hivyo itakuwa imeimarisha na kukuza fasihi ya Kiswahili nchini Tanzania. Mfano; tamthiliya ya JULIASI KAIZARI (Julius Caesar) (1963) na tamthiliya ya MABEPARI WA VENIS (The Merchant of Venis) (1969) iliyotafsiriwa na Mwalimu Julius K. Nyerere, WIMBO WA LAWINO (Song of Lawino) iliyotafsiriwa na Paul Sozigwa (1975), riwaya ya UHURU WA WATUMWA (The Freeing of the Slaves in East Africa) iliyotafsiriwa na East African Literature Bureau (1967), NITAOLEWA NIKIPENDA (I Will Marry When I Want) iliyotafsiriwa na Crement M. Kabugi (1982), Riwaya ya BARUA NDEFU KAMA HII iliyoandikwa na Mariama Bâ katika lugha ya kifaransa (Une si longue lettre) ikatafsiriwa katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili na Professor Maganga.
Pia tafsiri hutusaidia kujua itikadi ya mwandishi na pengine itikadi ya jamii husika. Kwa muktadha wa tamthilia ya Nitaolewa Nikipenda tunaona mwandishi anapinga sana tamaduni na  mtindo wa maisha ya kimagharibi ikiwa ni pamoja na dini za kigeni, lugha zao na mambo yote yaliyoletwa na Wakoloni mfano katika ukurasa wa tano (uk 5).



Kama unahitaji huduma ya kuandikiwa makala katika tovuti yako, au huduma yoyote basi wasiliana nami kupitia:-
SIMU:         +255 755 987 604, +255 789 198 345
E-MAIL:    reubentanzania@gmail.com



Hitimisho
Katika kazi hii tumeangalia vitabu vya Fasihi ya Kiswahili vilivyotafsiriwa, tumeangalia mchango wa Tafsiri katika Fasihi ya Kiswahili na kugusia kwa uchache mchango wa tafsiri katika Fasihi Linganishi. Kwa hiyo kulingana na kazi hii tunaweza kuona mchango na nafasi ya tafsiri katika taaluma ya Fasihi ya Kiswahili, hivyo kuna ulazima mkubwa kwa mtu anayeshughulika na Tafsiri awe ni mjuzi wa Fasihi, hii ni kwa lengo la kuzalisha zao bora la Tafsiri ya Kifasihi. Lakini pia kuna ulazima mkubwa kwa mtaalamu wa Fasihi Linganishi kujua taaluma ya Tafsiri kwa sababu anapofanya ulinganishi kati ya tafsiri na kazi za kifasihi ni lazima uwe na uelewa wa kutosha juu ya taaluma ya Tafsri. Kwa hiyo Fasihi Linganishi na Tafsiri kimsingi ni taaluma zinazoshikamana kuliko kuachana.






MAREJELEO
Mwansoko, H.J.M na wenzake (2006) .Kitangulizi cha Tafsiri, Nadharia na Mbinu. TUKI. Dar-es-salaam
Remak, H.H. (1971). Comperative literature: Its Definition and Function. Carbondale:  Southern Illinois.
Wamitila, K. W. (2003) Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publication
Wa Thiong’o, N. & Wa Mirii (1982). I Will Marry When I Want. East African Educatinal Publishers: Nairobi.
Wa Thiong’o, N. & Wa Mirii (1982). Nitaolewa Nikipenda. East African Educatinal Publishers: Nairobi.

MUINGILIANO KATI YA SEMANTIKI NA PRAGMATIKI---ACADEMICIAN BLOG

UTANGULIZI Maana ya Semantiki Richmond (2012   anafafanua maana ya Semantiki kwamba ni tawi la isimu ya lugha linalohusu viyambo ...