Jumanne, 27 Novemba 2018

UJASIRIAMALI--JINSI YA KUPATA MTAJI BILA KUKOPA

JINSI YA KUPATA MTAJI KWAAJILI YA KUANZISHA BIASHARA BILA KUKOPA (MKOPO)
Kabla ya kujifunza kitu chochote katika makala hii, ni vyema tukajuzana kuwa, biashara haihitaji haraka kama jinsi tunavyoichukulia biashara. Biashara inahitaji utaratibu wa hatua kwa hatua, huku ukifanya tathmini kwa kila hatua (yaani unaangalia mafanikio, changamoto,  mapungufu na namna ya kutatua vizuizi vinavyojitokeza katika biashara).
Mjasiriamali mdogo anashauriwa kuanza na mtaji mdogo na kisha kuukuza mtaji huo kidogo kidogo. Ni rahisi kufikia malengo yako kibiashara endapo kama utaona kila fedha inafaa kuwa mtaji kwa kuanza biashara. Kwa mfano, umepanga kuwa, baada ya miezi mitatu (3) inatakiwa upate shilingi 1,000,000/- (Milioni moja), ili kuanzisha biashara ya kusafirisha mazao kutoka vijijini na kuyapeleka mjini, huku ukiwa na shilingi 50,000/- (elfu hamsini) mfukoni  mwako. Lakini cha kushangaza, baada ya miezi mitatu ya malengo, unajikuta una shilingi 100,000/- (Laki moja tu) ama chini ya hicho kiasi. Kwa muonekano huo, utakuwa umefeli kabisa kupata shilingi 1,000,000/- kwaajili ya kuanzisha biashara ya kusafirisha mazao mjini.
# Kosa limetokea wapi?
Kimsingi fedha ya biashara haitakiwi kukaa bila kuzungushwa na kuleta faida. Kumbe basi, ilitakiwa ile ile shilingi 50,000/- (elfu hamsini) uitazame kama mtaji unaofaa kuanzisha biashara ndogo yenye uwezo wa kukupatia hata faida ya shilingi 15,000/- (elfu kumi na tano) kwa siku. Kuna biashara nyingi za kuweza kukupatia hicho kiasi cha pesa kwa siku endapo kama utakuwa tayari kufanya kazi kwa bidii na kujituma. Kwa mfano, unaweza ukaenda soko kuu lolote lililo karibu, kisha ukanunua matunda ya shilingi 50,000/- kwa bei ya jumla na kisha ukayauza kwa  wanaojua nini maana ya matunda, ungeweza kupata faida ya shilingi 20,000/- kwa siku Hii ingekujengea msingi na mwanzo mzuri katika safari yako ya kuitafuta shilingi 1,000,000/- kama mtaji wa kuanzisha biashara ya kusafirisha mazao kutoka vijijini na kuyapeleka mjini. Hii inawezekanaje? Tuangalie hesabu ndogo hapa chini.
Kwa masoko makubwa yaliyomengi nchini Tanzania, bei za jumla za matunda ni kama ifuatavyo;-
*      Chungwa  1= shilingi 100/=, na unaweza kuuza kwa bei ya machungwa 6 = shilingi 1,000/=
*      Maembe  3 (ya ukubwa wa wastani ya kati) = shilingi 500/=, na unaweza kuuza kwa bei ya shilingi 1,000/= (elfu moja, kwa fungu la maembe 3)
*      Tikiti maji 1 (la saizi ya kati) 2,000/= hadi 3,000/=, na ukaweza kuuza kwa bei ya shilingi 4,000/= hadi 5000/= (Isipokuwa kwa mikoa ya Dae-es-Salaam, Arusha, na Pwani) kwa upande wa Tanzania,
*      Parachichi 3 (za ukubwa wa wastani ya kati) = shilingi 500/=, na unaweza kuuza kwa bei ya shilingi 500/= kwa kila parachichi 1, au kwa bei ya shilingi 1,000/= kwa fungu la parachichi 3.
Je, hii siyo faida? Na pia, ngoja nikupe siri hii msomaji wangu! Hakuna biashara iliyonzuri kama biashara inayokupatia faida inayolingana na mtaji, au faida inayozidi mtaji uliowekeza, haijalishi ni kiasi gani cha mtaji ulichowekeza. Katika biashara, unapoongeza wateja wapya, ndivyo unavyoongeza faida zaidi na zaidi.
Kwa mchanganuo huu, nategemea kutosikia neno “sina mtaji” kwa msomaji wangu aliyesoma makala hii, kwani naamini kabisa kuwa, hakuna mtu ambaye anaweza kukosa shilingi 500/= ya kuanzisha biashara ya kuuza matunda kwa watu wanaojua umuhimu wa matunda.
Mtu anawezakuwa na uwezo wa kukusanya faida ya shilingi 50,000/= (elfu hamsini) kama faida ya siku moja, lakini asiwe na maendeleo yoyote. Donald  J.Trump, na Robert  T. Kiyosaki, katika kitabu chao kinachojulikana kama Why We Want You To Be Rich” katika masuala ya maendeleo kibiashara, walisema “Tatizo siyo kwamba tunaingiza shilingi ngapi, bali tatizon ni, tunatunza shilingi ngapi? Lakini pia wote kwa pamoja wanakubaliana kuwa, katika biashara, kwa waliowengi, “Tatizo siyo mtaji! Ila tatizo ni kukosa elimu ya biashara na ujasiriamali” nukuu za waandishi hawa zinadhihirisha ukweli kabisa kuwa, hata shilingi 1,000/= (elfu moja) ni mtaji tosha wa kuanziasha baadhi ya biashara, ila shida kubwa ni kuifanya hiyo shilingi 1,000/= izae na kuleta mtaji mkubwa zaidi.

# ANGALIZO KWA MJASILIAMALI MDOGO (MUUZAJI WA MATUNDA)
Ø  Kama una mtaji mdogo, chonde chonde usifanye biashara ya kusafiri umbali mrefu, bali fanya biashara ya kusafiri kwa umbali usiozidi lisaa limoja. Hii itakurahisishia kuwa na uhakika wa kurudia bidhaa muda wowote utakapomaliza bidhaa, na hivyo kufanya mzunguko wako kwenda haraka,  wenye tija na wenye kukupatia faida zaidi.
Ø  Usikopeshe zaidi ya nusu ya mtaji wako, maana kwa kufanya hivyo, unaweza ukajikuta unakosa fedha ya kwenda kuchukulia mzigo, wakati ukiwa umeshauza mzigo wote (ila kwa mkopo).
Ø  Mkopeshe mteja ambaye una uhakika wa kulipwa ndani ya masaa kadhaa, na siyo siku kadhaa.
Ø  Uwe mwaminifu na mkweli katika biashara zako
Ø  Itetee vyema biashara yako
Ø  Ipende biashara yako, kwa kuiona kama ndiyo kazi yako uliyoajiriwa.
Ø  Uwe na lugha nzuri kwa wateja wako! hata kama hutaki kumkopesha, si vyema ukamwambia kuwa “sikopeshi” badala yake mwambie “kwa kweli leo sina hela ya kwenda kuchukulia mzigo, mzigo huu ndio ninaoutegemea kuongezea mtaji wa leo” mteja huwa ni mwelewa sana endapo kama utatumia lugha ya kumwelewesha kwa utaratibu na bila kuharibu furaha yake aliyonayo siku hiyo.
Ø  Kuwa na bei rafiki na isiyomuumiza mteja (yaani unakuwa na watja wa kila aina, wapo wale wenye uwezo mzuri, pia wapo ambao uwezo wao ni mdogo, ila kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao,inawabidi wapate bidhaa zao ili maisha yaende) kwa mfano, kwa mjasiriamali anayeuza matunda, atakutana na wateja kama vile wagonjwa, wajawazito na wamama waliojifungua siku si nyingi. Hawa wote wanahitaji huduma ya matunda, hivyo ni vyema kwa muuzaji kujua saikolojia na uwezo wa wateja wake.

Nakushukuru kwa kufuatilia makala zangu katika blog yangu na katika kurasa zangu za mitandao ya kijamii. Usikose kufuatilia makala zangu zingine, ni rahisi sana, ingia kwenye blog yangu kisha bofya kitufe  follow  by e-mail. Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kupata makala zangu mpya.

REJEA
Trump, D.J & Kiyosaki, R.T (2006) Why We Want You To Be Reach. Rich Press
                        Publishers.New York.

Maoni 23 :

  1. Shukran ndg yaani umefafanua kwa uzuri zaidi hadi mimi kichwa ngumu nimeelewa. Ahahahaaaa!!!! Ahsante sana

    JibuFuta
    Majibu
    1. asante nawe kwa kusoma makala hii! naamini utakuwa umepata kitu kutoka katika makala hii.

      Futa
    2. Sikuwahi kuamini kitu kama hiki kingeweza kunitokea hadi ndoa yangu ilipokaribia kuisha kabisa.

      Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
      Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
      Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.

      Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
      Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
      Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
      Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
      Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
      Nitaendelea kushukuru milele.
      Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
      . Usaidizi wa kurejesha ndoa
      . Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
      . Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
      . Mwongozo na ulinzi wa kiroho
      Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159

      dawnacuna314@gmail.com

      Futa
  2. Aise sijawai toa comment ktk blog leo umenishawishi vizuri broo

    JibuFuta
    Majibu
    1. ndivyo ilivyo kka, kufanikiwa kibiashara, siyo jambo la kulala na ukaamka tajiri! bali inahitajika kujituma zaidi na kuheshimu mtaji ulionao.

      Futa
  3. Nimeukubali ushauri na nitaufanyia kazi

    JibuFuta
    Majibu
    1. vizuri! hatua moja ndiyo husababisha kutokea kwa hatua nyingine!

      Futa
  4. Dah, umenifumbua macho mwandishi, asante tukutane 2020

    JibuFuta
    Majibu
    1. Mungu atusaidie, ili 2020 iwe ni mwaka wa mafanikio

      Futa
  5. Nimeongeza kitu kikubwa sana asante sana

    JibuFuta
    Majibu
    1. elimu ya biashara siyo hadi tufike chuo kikuu, bali ni kile unachokutananacho katika katika biashara unayoifanya na katika maisha kwa ujumla! KILA PESA NI MTAJI, kama mtu anatoka nyumbani na Tsh. 1000 anaenda mnadani kudaka mkanda mmoja, na kisha anautembeza na kuuuza Tsh 2000 hadi Tsh. 5000, hapo hajapata faida???

      Futa
  6. Nimeongeza kitu kikubwa sana asante sana

    JibuFuta
  7. Natarajia kuanza bishara hii mwezi wa 3/2020. Najua changamoto zipo. Swali! Je utakuwa tayari kunisaidia kimawazo pind nahitaji ushauri? katika kuhoresha na katika changamoto pia.

    JibuFuta
    Majibu
    1. Bila shaka, nipo tayari tumia 0755482030

      Futa
  8. Asnt kw ufafanuzi
    Barikiwa san

    JibuFuta
    Majibu
    1. Asante, nawe barikiwa pia kwa kupokea kipya ki mawazo

      Futa
  9. Asanten sana. Mmenifanya nikafahamu kitu kwenye biashara. Naweza kupata group lenu la whatsap??

    JibuFuta
  10. Naomba namba za whatsap?

    JibuFuta
  11. Nimekuelewa sana kaka umefafanua vizuri sana nimependa sana

    JibuFuta
  12. Natamani kupata mawasiliano yako Moja kwa Moja mana nimeupenda mafundisho yako

    JibuFuta
  13. Sikuwahi kuamini kitu kama hiki kingeweza kunitokea hadi ndoa yangu ilipokaribia kuisha kabisa.

    Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
    Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
    Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.

    Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
    Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
    Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
    Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
    Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
    Nitaendelea kushukuru milele.
    Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
    . Usaidizi wa kurejesha ndoa
    . Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
    . Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
    . Mwongozo na ulinzi wa kiroho
    Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159

    dawnacuna314@gmail.com

    JibuFuta

MUINGILIANO KATI YA SEMANTIKI NA PRAGMATIKI---ACADEMICIAN BLOG

UTANGULIZI Maana ya Semantiki Richmond (2012   anafafanua maana ya Semantiki kwamba ni tawi la isimu ya lugha linalohusu viyambo ...