Jumamosi, 2 Desemba 2017

MUINGILIANO KATI YA SINTAKSIA, MOFOLOJIA NA FONOLOJIA,


A. Muingiliano kati ya Sintaksia na Mofolojia (Mofo-Sintaksia)
Rubanza (1996) anasema, mofolojia ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha katika kuunda maneno.
(Rubanza, 1996) anatupatia muingiliano wa sintaksia na mofolojia kama ifuatavyo:-
kipashio cha msingi katika uchambuzi wa kimofolojia ni neno ambalo, ambalo pia hutumika kuunda darajia ya sintaksia. Pia maumbo ya kimofolojia huathiri vipengele vingine vya kisintaksia
Mfano:           ( i ) M-toto  a-napika (umoja)             
(ii ) Wa-toto  wa-napika (wingi)
Katika mifano hii, tunaona kwamba mofimu //m//  na //wa// katika upande wa kiima zimeathiri utokeaji wa “a”- na “wa” katika upande wa kiarifu.

Pia kanuni za mfuatano wa mpangilio wa mofimu au viambishi zikifuatwa huunda maneno katika miundo ya kisintaksia.
Mfano:           Alioga     A – li – og – a
Analiona →  A- na – lim- a

Hivyo kipengele cha umoja na uwingi katika maumbo ya kimofolojia ndicho kinacho athiri umbo linalofuata jina na kuathiri muundo wa sentensi nzima
Mfano:           Mganga anaandika barua
                                 Waganga wanaandika barua

Matinde (2012) na Habwe  & Karanja (2004) katika maelezo yao wanatupatia muingiliano uliopo baina ya sintaksia na mofolojia kama ifuatavyo:-

1. Mofolojia ndio inayotupatia kizio kidogo kabisa cha kisintaksia, hii ina maana kuwa, kuna baadhi ya dhana ambazo hutumika katika matawi yote mawili ya kisarufi yaani mofolojia na sintaksia, mfano “neno”, hiki ni kizio cha juu kabisa cha mofolojia lakini pia neno ndicho kizio kidogo kabisa cha sintaksia.

2. mofimu huru ndizo huungana na kutupatia viwango mbalimbali vya kisintaksia kama vile kirai, kishazi, tungo na hata sentensi.
Mfano:           //Baba//  + //yetu// →  Baba yetu (kirai)
                                     //Gari// + //zuri//     Gari zuri  (kirai)
                                      //Juma// + //Cheza// + //mpira// → Juma cheza mpira (sentensi)

3. Sintaksia na mofolojia huingiliana kupitia dhana ya urejeshi, ambapo kunakuwa na viambishi (Mofolojia) hurejea umbo lingine katika sentensi (sintaksia) na kufanya pawe na uhusiano baina ya maumbo hayo.
Mfano:            Chatu aliyepita hapa ameuawa.
Mtoto  aliyejichoma kisu amefariki.
Jembe  lililonunuliwa limepotea

Hapa tunaona maumbo ya urejeshi ya “ye” na “lo” yanarejerea mtenda. Kwa upando mwingine umbo la “ji” linarejerea kifaa kilichotumika katika tukio. Kwa ujumla maumbo ya urejeshi ndio yanayolazimisha kutokea kwa maumbo mengine katika sentensi au tungo ili kukamilisha dhana inayozungumziwa.

4. Kuna baadhi ya maumbo (mofolojia) hayawezi kuwa na maana yoyote endapo kama yatasimama peke yake, lakini maumbo hayo hayo  yakiambatanishwa na maneno mengine katika sentensi huweza kupata maana. Maumbo hayo ni kama vile vihusishi “ya”, “la”, “ya”, “na”, “ni”, “kwa” na “kama”.
Mfano:           Gari la juma (“la” lina maana ya umilikishi).
                                    Mutachuba na wadugu wanaimba (“na” – kiunganishi).
Mzilani atasafiri kesho kama atapata ruhusa (“kama” ina maana ya uwezekano).
                                     Asha anatembea kwa miguu (“kwa” – namna tendo linavyofanyika).
                                     Juma ni mwizi (“ni” inathibitisha kuwepo kwa tabia).
                                     Kompyuta ya baba (“ya”- kimilikishi).  

5.  Kuna baadhi ya maumbo (mofolojia) huweza kubadili sentensi (sintaksia) kutoka hali moja na kwenda hali nyingine.
Mfano:           1    (a) Huyu ni mwizi (ni- hali yakinifu)
                                          (b) Huyu si mwizi  (si – hali kanushi)
                                     2.  (a)  Mtoto anaimba  (na - hali iliyopo)
                                          (b)Mtoto ameimba  (me – hali timilifu)
                                     3   (a)Juma aliimba akapewa zawadi
(b)Juma angeimba angepewa zawadi (“nge” imebadili kabisa    mauombo katika sentensi hii)

6. Dhana ya uelekezi; sintaksia na mofolojia huingiliana kupitia uelekezi. Uelekezi ni hali ya kitenzi kuruhusu au kutoruhusu nomino kufuata mbele yake (Matinde, 2012). kuna baadhi ya maumbo (mofolojia) hususani vinyambuzi vinapowekwa katika kitenzi, huweza kuamua kuwa ni idadi za nomino  kufuata ama kutofuata kabisa.
Mfano:  ( i ) Dada amempik- i- a  baba chakula (nomino mbili).
 Hapa tunaona umbo (kinyambuzi) “ i ” kimeruhusu nomino mbili kufuata baada ya kitenzi.
                           ( ii ) Baba amempig – a  mwizi
                                     Hapa pia tunaona kinyambuzi “a” kimeruhusu nomino moja kufuata.  
7. Kiambishi ngeli (mofolojia) huweza kuathiri utokeaji wa maumbo ngeli mengine katika sentensi (sintaksia). Hii ina maana kuwa maumbo ngeli (mofolojia) kwa kiasi kikubwa hutawala maumbo mengine katika sentensi (sintaksia)
Mfano: (i) M-toto a-nacheza (“m”-umbo ngeli lenye kubeba dhana ya umoja ndilo lililopelekea kutokea kwa “a” katika kitenzi anacheza
(ii) Wa-toto wa-nacheza (“wa”- ni umbo ngeli 2, lenye kubeba dhana ya wingi       na ndilo lililopelekea utokeaji wa umbo “wa” katika kitenzi wanacheza.
(iii)  Mwalimu alikuwa anafundisha
(iv)  Walimu walikuwa wanafundisha
Tunaona katika mifano hii maumbo ya umoja na uwingi wa maneno mwalimu na walimu yameathiri mpangilio mzima wa sentensi 



Maumbo ngeli (mofolojia) kwa kiasi kikubwa ndiyo yanayoleta upatanisho wa kisarufi katika sentensi (kisintaksia).

8. Kuna mabadiliko ya kimofosintaksia ambayo hutokea kwa kuhusisha dhana zote mbili za sintaksia na mofolojia. Kwa kiasi kikubwa mabadiliko haya hutokea ili kuleta upatanisho wa kisarufi katika tungo. Neno moja katika sentensi linaweza pelekea mabadiliko katika neno lingine linalofuata.
Mfano:       (i) Mtoto uake →mtoto  u     a ke
                                                        Wake
 
(ii) Miaka    iake → Miaka      i       a ke

                                                Yake
Mtoto mudogo  - mtoto  mu  dogo
                              Mtoto     mdogo
Katika mifano hapo juu, tunaona mabadiliko mbalimbali yametoke. Katika mfano (i) tunaona neno “mtoto” limepelekea badiliko la uyeyushaji wa irabu “u” na kuwa “w” na kupata neno “wake” badala ya “uake”. Katika mfano (ii) pia tunaona badiliko la irabu “ i” kuwa “y” kutokana na uyeyushaji, hivyo tunapata neno “yake” baada ya “iake”. Lakini pia katika mfano (iii) tunaona badiliko la kupunguzwa kwa “u” kati ya “m” na “d”, badiliko hili linatokana na udondoshaji uliofanyika ili kuleta urahisi katika kukitamka kirai “mtoto mdogo”
Habwe na karanja (2004) katika maelezo yao, wanaongeza baadhi ya muingiliano kati ya mofolojia na sintaksia kama ifuatavyo:-

9. Sintaksia na mofolojia huingiliana katika utendaji; kuwa vyote hujihusisha na kuchunguza mpangilio katika Lugha. Mofolojia huchunguza mpangilio wa mofu katika neon, wakati sintaksia huchunguza mpangilio wa maneno katika sentensi.

10 sintaksia na mofolojia kwa pamoja huhusisha au hutumia taratibu (hatua) za kisayansi katika uchunguzi wa lugha ya binadamu.
11. Sintaksia na mofolojia kwa  pamoja huchunguza muundo wa ndani na muundo wa nje wa lugha. Mofolojia kwa upande wake huchunguza muundo wa ndani na muundo wanje wa maneno katika lugha (Matinde, 2012).
Mfano.
Neno
Muundo wa ndani
Muundo wa nje
Mutu
Mutu
Mtu
Mbwa
Mmbwa
Mbwa
Nje
Nnje
Nje

Katika upande mwingine sintaksia huchunguza muundo wa ndani na muundo wa nje wa sentensi (sintaksia)
Mfano:  (i)      Juma cheza mpira (muundo wa ndani)
                                     Juma anacheza (muundo wan je)
                         (ii)      Asha anacheza vizuri mpira wake (muundo wan je)
                                     Asha anacheza mpira wake vizuri (muundo wa ndani)
12. Kwa baadhi ya dhana kama vile virejeshi (mofolojia) zikitumika katika sentensi huweza kuibadili sentensi sahili na kuwa sentensi tegemezi (kishazi tegemezi)
Mfano:   (a)  Mtoto anasoma kitabu (sentensi sahili)
                         Mtoto anayesoma kitabu (kishazi tegemezi)
    (b)   kiti kimevunjika (sentensi sahili)
                         Kiti kilichovunjika (kishazi tegemezi)
  (c),   kuku amenunuliwa (sentensi sahili)
                         Kuku aliyenunuliwa (kishazi tegemezi)


B. Muingiliano kati ya Sintaksia na Fonolojia (Mofo-Fonolojia)

1.Uhusiano baina ya fonolojia na sintaksia, Massamba na wenzake (wameshatajwa) wanafasili fonolojia kuwa ni uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha zinavyoungana ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha kwa hiyo tunaweza kusema kuwa kuungana kwa vitamkwa ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha fulani hutegemea mpangilio sahihi wa vitamkwa. Na kwa kuwa neno ni kiwango cha msingi cha uchambuzi katika sintaksia, basi fonolojia inauhusiano wa moja kwa moja na sintaksia.
Mifano ifuatayo huthibitisha hoja hii
(I)                “Anapika” hii ni neno lakini pia ni sentensi hivyo huweza kuchanganuliwa kifonolojia kama ifuatavyo  a/n/a/p/i/k/a/, mpangilio wa sauti umeunda neno “anapika”.
(II)             (a)  baba limeundwa na ( limeundwa kwa muundo wa silabi wa KIKI)
(b)   Abab limeundwa na ( limeundwa kwa IKIK)
Katika mfano 2a tunaona neno “baba” lina maana na limefuata kanuni na mpangilio unaokubalika wakati mfano 2b neno abab halina maana katika lugha ya Kiswahili kwa sababu halina mpangilio mzuri wa fonimu. Kwa mifano hii tunaona kwamba, hatuwezi kuwa na miundo mikubwa katika sentensi bila kuwa na mpangilio sahihi wa sauti katika lugha. kwa hiyo sintaksia haiwezi kukamilika bila fonolojia.

2. Fonolojia pia ndiyo chimbuko la sentensi kwani, sauti (konsonanti na irabu) ndizo huungana na kutupatia neno (maneno) ambayo ndiyo huungana kutupatia kirai, kishazi na hata sentensi ambavyo hivi vyote ni viwango vya kisintaksia (Nchimbi, 2008) 

3. Pia kanuni za mfuatano na mpangilio wa mofimu au viambishi zikifuatwa huunda maneno katika miundo ya kisintaksia mfano.
(i)                 Alicheza = a-li-chez-a
(ii)               Anaimba  = a- na- imb-a


Kama unahitaji huduma ya kuandikiwa makala katika tovuti yako, au huduma yoyote basi wasiliana nami kupitia:-
SIMU:         +255 755 987 604, +255 789 198 345
E-MAIL:    reubentanzania@gmail.com


 MAREJEO
Massamba D.PB na wenzake (1999) Sarufi miundo ya Kiswahili sanifu: Sekondari na vyuo.
 Dar  es salaam.TUKI.  
Rubanza Y.I (1996) Mofolojia ya Kiswahili: Dar es salaam: Chuo kikuu huria cha Tanzania. 
 TUKI (2004) Kamusi ya Kiswahili sarufi: Dar es Salaam.TUKI.
 Nchimbi A. S (2008) OFC, Kiswahili: Dar es Salaam. Chuo kikuu Huria cha Tanzania.
Habwe J. & Karanja P.C (2004) Misingi ya sarufi ya Kiswahili:Nairobi. Phoenix Publishers Ltd.
Matinde R.S (2012) Dafina ya lugha Isimu na Nadharia kwa Sekondari, Vyuo vya kati na vyuo vikuu :Mwanza. Serengeti education publishers (T) Ltd. 
Massamba,D.P.B na Wenzake (2004) Fonolojia ya Kiswahili (FOKISA), Sekondari na Vyuo:
                            Dar es salaam Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI).

Maoni 22 :

  1. Jamani! kwanini somo la Kiswahili huonekana kama gumu sana kwa baadhi ya wanafunzi wa upili hasa kwa kidato cha 5 an 6?

    JibuFuta
    Majibu
    1. wao hupendelea sana lugha ya kigeni...na kutopenda kiswahili

      Futa
  2. Hii Ni kwa sababu baadhi ya wanafunzi wao wameathiriwa na lugha ya kwanza kabisa.Hii ndiyo sababu huenda wakaiona somo La kiswahili kuwa mgumu

    JibuFuta
  3. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  4. Usitume free domain kama. Blogspot.com na za wordpWord.com tengeneza yako mwenyewe upige hella. Ntafte nkuelekeze

    JibuFuta
  5. beast, tupia namba yako nikuchek

    JibuFuta
    Majibu
    1. samahan ndugu yangu kwa kuchelewa kujibu ujumbe wako! namba yangu ni 0755987604

      Futa
  6. safi sana, naandaa nyuzi nyingine!

    JibuFuta
  7. Ningependa kutambua uhusiano Kati ya fonolojia na mofolojia

    JibuFuta
    Majibu
    1. Usijal ndg, muda si mrefu ntachapisha makala juu ya uhusiano wa Fonolojia na Mofolojia

      Futa
  8. Naomba kufahamu kuhusu michakato na kanuni za kimofo-fonolojia/kimofo-fonemiki!

    JibuFuta
  9. Kuna sina ngap za maneno? Tuma wataalam watano

    JibuFuta
  10. Naomba unipatie ufanano wa fonetiki na fonoloji angalau pointi tano(5)

    JibuFuta
  11. Naomba uhusiano kati ya fonolojia na sintaksi.hoja (5)

    JibuFuta
  12. Nitmie hyo makala kiongozi

    JibuFuta
  13. Makala nzuri naomba kutumiwa kikashani

    JibuFuta
  14. Kwa kutolea ithibati ya kiisimu, ningependa unisaidie na uhusiano uliopo baina ya fonolojia na mofolojia

    JibuFuta

MUINGILIANO KATI YA SEMANTIKI NA PRAGMATIKI---ACADEMICIAN BLOG

UTANGULIZI Maana ya Semantiki Richmond (2012   anafafanua maana ya Semantiki kwamba ni tawi la isimu ya lugha linalohusu viyambo ...