CHUO KIKUU
KISHIRIKI CHA ASKOFU MKUU YAKOBO
KITIVO CHA SANAA NA SAYANSI ZA JAMII
IDARA YA LUGHA, ISIMU NA FASIHI
JINA LA KOZI :
MOFOLOJIA YA KISWAHILI
MSIMBO WA KOZI :
SW 232
JINA LA MHADHIRI :
SOTE, A
AINA YA KAZI : KAZI YA KIKUNDI
YA SEMINA
KUNDI :Na. 08
MAJINA.
Na
|
JINA
|
NAMBA YA USAJILI
|
SAHIHI
|
01
|
BUYA FADHILI, A
|
BAED2 45283
|
|
02
|
KINUNDA JOSEPH
|
BAED2 45332
|
|
03
|
KITIKITI MARIAM
|
BAED2 45334
|
|
04
|
KOMBA ADELHEMA
|
BAED2 45337
|
|
05
|
MBUNDA CLEMENCE, L
|
BAED2 45360
|
|
06
|
MTEGA
THEOBIAS, T
|
BAED2 45383
|
|
07
|
MYOMBE BARAKA
|
BAED2 45402
|
|
08
|
REUBEN JOHN,K
|
BAED2
45431
|
|
09
|
NGIMBA SHAADA
|
BAED2 45469
|
SWALI: JADILI KWA HOJA
NA MIFANO NDUNI ZA UNYAMBULISHAJI.
UTANGULIZI
Kwa
ujumla kazi hii ina sehemu kuu tatu, ambazo ni Utangulizi, Kiini cha kazi na
Hitimisho. Utangulizi una husisha maana ya Unyambulishaji kutokana na mawazo ya
wataalamu mbalimbali na Maana ya Wanakikundi juu ya Unyambulishaji. Sehemu ya
pili inahusu Kiini cha kazi hii, ambapo Nduni zipatazo tisa zimeweza kujadiliwa
zikiwa na mifano yake, na Sehemu ya tatu ni hitimisho, ambalo limebeba maoni
kuhusu jinsi ya kutofautisha dhana ya Unyambulishaji na Uambishaji (Uambatizi).
Maana ya Unyambulishaji kwa mujibu
wa mawazo ya Wataalamu mbalimbali.
BAKIZA
(2010) wanasema kuwa Unyambulishaji ni muendelezo wa shina la neno kwa
kuongezea viambishi ili kujenga neno jipya.
Kihore
(2009) naye anasema kuwa, unyambulishaji
ni tendo la kupachika vipashio kwenye kiini ili kujenga (ma) neno.
Unyambulishaji
ni utaratibu wa kupachika viambishi kwenye mzizi ili kuunda maneno mapya
(Massamba, 2004).
Hivyo
basi, Unyambulishaji ni tendo la kuongeza viambishi katika mzizi wa neno yaani
kabla ya mzizi au baada ya mzizi wa neno, ambapo matokeo yake yaweza kuwa ni
kubadili maana ya neno, kategoria ya neno au yawezakuwa kubadili aina ya neno
ndani ya kategoria moja ya neno.
NDUNI ZA UNYAMBULISHAJI
TUKI
(2013) Wanatupatia maana ya neno “Nduni” kuwa, ni “sifa maalumu ya kitu”. Kwa
maana hiyo basi, Nduni za Unyambulishaji ni sifa za unyambulishaji, na
zifuatazo ni nduni za Unyambulishaji kwa mujibu wa Nchimbi (2008).
1. Unyambulishaji
unatokea au unafanyika katika kategoria za maneno au katika maneno yanayokubali kubadili umbo
lake. Hii ikiwa na maana kuwa, maneno yanayokubali kupokea mofu mbalimbali
katika umbo lake .
Mfano.
Mtoto
> ki-toto, Tu-toto
Bakuli > ki-bakuli, vi-bakuli
Taifa
> M-taifa, U- taifa, ki-taifa.
Kwa upande mwingine unyambuzi hauwezi kutokea au
kufanyika katika maneno yasiyokubali kubadili umbo lake.
Mfano.
Viunganishi : na, kwa, katika, au, pia
Vihisishi : Mfano, loo !, ewe !, la
hasha !
Vihusishi : Mfano, la, ya, cha, kwa
Vielezi asilia : Mfano, mapema, asubuhi, sana
2.
Maneno
yanayoundwa kutokana na unyambulishaji yanaweza kupewa maana ama mpya au maana
ya ziada. Kwa mantiki hii, kumbe unyambulishaji unaweza kubadili maana ya neno,
kwa kutoa matokeo ya maana mpya ya neno.
Mfano.
Chumba > Chumba-ni
Pig-a > Pig-o
Taifa > U-taifa
Kasuku > U-kasuku
Jiko > U-jiko
3.
Unyambulishaji
unaweza kubadili kategoria ya neno, kutoka katika kategoria moja na kwenda
katika kategoria nyingine ya neno.
Mfano.
Kutoka kategoria ya Kitenzi kwenda
kategoria ya Nomino.
Pig-a > Pig-o,
Pig-an-o
Tuli-a > M-tulivu
Karibisha > M-karibishaji
Sawazisha
> Sawaz-ish-o
Kutoka kategoria ya Kielezi kwenda
kategoria ya Kitenzi
Mfano.
Rahisi > Rahis-ish-a
Karibu > Karib-i-a, Karib-ish-a
Sawa >
Sawaz-ish-a
Kutoka kategoria ya Nomino kwenda kategoria
ya Kielezi
Mfano.
Katiri
> Ki-katiri
Chumba
> Chumba-ni
Mzalendo
> Ki-zalendo
Afande
> Ki-afande.
Kutoka kategoria ya Kivumishi kwenda kategoria ya Kitenzi
Mfano.
Fupi
> Fupisha
Nene
> Nenepesha
Bora
> Boresha.
4. Unyambulishaji
pia unauwezo wa kubadili aina ya neno katika kategoria moja . Hii ina maana
kuwa ndani ya kategoria moja ya neno, Neno linaweza kubadilishwa aina kutoka
aina moja ya neno na kwenda aina nyingine ya neno pasipo kuathiri au kubadili
kategoria ya neno husika. Kwa mfano, Katika kategoria ya Nomino, Neno linaweza
kubadilishwa kutoka katika aina ya nomino za kawaida na kuwa nomino dhahania.
Mfano.
Chumba
> U- chumba
Jiko
> U-jiko
Mzee
> U-zee
Jambazi
> U-jambazi
Kenge > U-kenge.
5. Unyambulishaji
una uwezo wa kuonyesha kauli katika kitenzi husika, na kumfanya mtumia lugha
atambue kuwa ni dhana gani inayozungumziwa au inayofanyika katika kitenzi.
Hivyo kupitia mnyambuliko tunaweza kupata kauli zifuatazo:-
Kauli ya kutenda:
Mfano, Pig-a, Som-a, Imb-a.
Kauli ya
Kutendwa: Mfano,
Pig-w-a, Som-w-a, Imb-w-a
Kauli ya Kutendana: Mfano, Pig-an-a, Imb-an-a.
Kauli ya
Kutenduka: Mfano,
Tega > Teg-u-a, Fumba > Fumb-u-a
Kauli ya
Kutendesha: Mfano, Imb-ish-a, Som-esh-a, Pig-ish-a.
6. Unyambulishaji
unaweza kubadili nafasi ya neno katika muundo wa kishazi au sentensi. Hii ina
maana kuwa, neno linaweza kuwa katika nafasi ya nomino katika sentensi, Lakini
baada ya neno hilo kufanyiwa unyambulishaji, neno hilo hilo linaweza kubadilika
na kuchukua nafasi ya kitenzi katika sentensi.
Mfano.
Juma
ana utaifa wa Marekani
Ø Utaifishaji
wa Juma ni wa Kimarekani
Katika
mfano huu tunaona jinsi ambavyo neno “utaifa” lilivyoweza kubadilishwa nafasi yake katika
sentensi.
Mbali
na nduni za Unyambulishaji zilizotolewa na Nchimbi (2008), Lakina pia Unyambulishaji
una nduni nyingine kama vile:-
7. Unyambulishaji
pia una sifa ya kuwa na vighaili vingi. Hii ikiwa na maana kuwa , Si kila neno
linakubali kuchukua kinyambuzi cha aina ile ile iliyotumika katika maneno
mengine.
Mfano.
a) Tung-a > Tung-o,
b) Teg-a >
Teg-o
c) Imb-a > Imb-o
d) Ib-a >
Ib-o
Tunaona
katika mfano ( c ) na ( d ) Maneno Imba na Iba yameshindwa kuendana na kanuni
ya maneno ya mfano ( a ) na ( b ). Hivyo maneno ya mfano ( c ) na ( d ) ni
vighaili katika kanuni iliyotumika katika mifano hii.
8. Vinyambuzi
pia siyo zalishi, Hii ikiwa na maana kuwa Vinyambuzi havina tabia ya kujirudia
rudia katika neno, na kuwa siyo kila neno linaweza kuambatanishwa na kinyambuzi
fulani na kuleta maana.
Mfano
Tenda
> Tend-an a,
Penda >
Pend-an-a
Kaa
> Ka-an -a
Lia > Li-an-a
Katika
mifano hii, tunaona jinsi ambavyo kinyambuzi –an- kisivyokuwa zalishi, Kwani kimeshindwa kutumika na kuleta maana
katika mfano wa ( iii ) na ( iv ) kama jinsi tulivyoona katika mifano hii.
9. Kwa
kiasi kikubwa sana, Kinyambuzi au vinyambuzi hutokea karibu sana na mzizi wa
neno. Ukaribu huu waweza kuwa kabla ya mzizi au baada ya mzizi wa neno.
Mfano.
Piga > Pig-an-a
Tulia
> M-tulivu
Mtoto
> ki-toto
Kama unahitaji huduma ya kuandikiwa makala katika tovuti yako, au huduma yoyote basi wasiliana nami kupitia:-
SIMU: +255 755 987 604, +255 789 198 345
E-MAIL: reubentanzania@gmail.com
HITIMISHO
Dhana
ya Unyambulishaji imekuwa ikichanganywa sana na dhana ya Uambishaji (Uambatizi),
ijapokuwa matendo haya yote yanahusisha kuongeza viambishi katika mzizi wa
neno. Lakini inapaswa tujue kuwa matendo haya yanatofautiana katika uamilifu
wake katika isimu ya lugha. Na utofauti huo unatokana na ukweli kuwa
Unyambulishaji unahusu kuongeza viambishi katika mzizi wa neno, wakati huo
viambishi hivyo vinakuwa na uamilifu wa kuunda neno jipya kutoka katika neno
lililofanyiwa unyambulishaji. Kwa upande mwingine, Uambishaji (Uambatizi)
wenyewe unahusiana na kuboresha maana ya mzizi wa neno kwa kubeba viambishi
vyenye kuchukua dhana ya idadi, nafsi, njeo na dhamira.
MAREJEO
Akmajian,
A et al (2001) LINGUISTICS, An
Introduction to Language and Communication
5thEd.USA:Massachusette
Institute of Technology Press.
BAKIZA (2010) Kamusi ya Kiswahili Fasaha.Nairobi:Oxford University Press,East
Africa L.t.d
Kihore,Y.M
(2009) Sarufi maumbo ya Kiswahili Sanifu
(SAMAKISA) Sekondari na Vyuo.
Dar es Salaam:Taasisi ya Uchunguzi
wa Kiswahili (TUKI).
Massamba,D.P.B
(2004) Kamusi ya Isimu na Falsafa ya
Lugha.Dar –es-Salaam:Taasisi ya
Uchunguzi wa Kiswahili.
Nchimbi,A.S
(2008) OFC 008 KISWAHILI.Dar es
Salaam:Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
TUKI
(2013:420) Kamusi ya Kiswahili Sanifu,
Toleo la 3.Nairobi:Oxford University Press.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni