JINSI YA KUPATA MTAJI KWAAJILI YA KUANZISHA
BIASHARA BILA KUKOPA (MKOPO)
Kabla ya
kujifunza kitu chochote katika makala hii, ni vyema tukajuzana kuwa, biashara
haihitaji haraka kama jinsi tunavyoichukulia biashara. Biashara inahitaji utaratibu
wa hatua kwa hatua, huku ukifanya tathmini kwa kila hatua (yaani unaangalia
mafanikio, changamoto, mapungufu na
namna ya kutatua vizuizi vinavyojitokeza katika biashara).
Mjasiriamali
mdogo anashauriwa kuanza na mtaji mdogo na kisha kuukuza mtaji huo kidogo
kidogo. Ni rahisi kufikia malengo yako kibiashara endapo kama utaona kila fedha
inafaa kuwa mtaji kwa kuanza biashara. Kwa mfano, umepanga kuwa, baada ya miezi
mitatu (3) inatakiwa upate shilingi 1,000,000/- (Milioni moja), ili kuanzisha
biashara ya kusafirisha mazao kutoka vijijini na kuyapeleka mjini, huku ukiwa
na shilingi 50,000/- (elfu hamsini) mfukoni
mwako. Lakini cha kushangaza, baada ya miezi mitatu ya malengo,
unajikuta una shilingi 100,000/- (Laki moja tu) ama chini ya hicho kiasi. Kwa muonekano
huo, utakuwa umefeli kabisa kupata shilingi 1,000,000/- kwaajili ya kuanzisha
biashara ya kusafirisha mazao mjini.
# Kosa limetokea wapi?
Kimsingi
fedha ya biashara haitakiwi kukaa bila kuzungushwa na kuleta faida. Kumbe basi,
ilitakiwa ile ile shilingi 50,000/- (elfu hamsini) uitazame kama mtaji unaofaa
kuanzisha biashara ndogo yenye uwezo wa kukupatia hata faida ya shilingi 15,000/-
(elfu kumi na tano) kwa siku. Kuna biashara nyingi za kuweza kukupatia hicho
kiasi cha pesa kwa siku endapo kama utakuwa tayari kufanya kazi kwa bidii na
kujituma. Kwa mfano, unaweza ukaenda soko kuu lolote lililo karibu, kisha
ukanunua matunda ya shilingi 50,000/- kwa bei ya jumla na kisha ukayauza kwa wanaojua nini maana ya matunda, ungeweza kupata
faida ya shilingi 20,000/- kwa siku Hii ingekujengea msingi na mwanzo mzuri
katika safari yako ya kuitafuta shilingi 1,000,000/- kama mtaji wa kuanzisha
biashara ya kusafirisha mazao kutoka vijijini na kuyapeleka mjini. Hii
inawezekanaje? Tuangalie hesabu ndogo hapa chini.
Kwa masoko makubwa yaliyomengi nchini
Tanzania, bei za jumla za matunda ni kama ifuatavyo;-




Je, hii
siyo faida? Na pia, ngoja nikupe siri hii msomaji wangu! Hakuna biashara iliyonzuri
kama biashara inayokupatia faida inayolingana na mtaji, au faida inayozidi
mtaji uliowekeza, haijalishi ni kiasi gani cha mtaji ulichowekeza. Katika biashara,
unapoongeza wateja wapya, ndivyo unavyoongeza faida zaidi na zaidi.
Kwa mchanganuo
huu, nategemea kutosikia neno “sina mtaji”
kwa msomaji wangu aliyesoma makala hii, kwani naamini kabisa kuwa, hakuna mtu
ambaye anaweza kukosa shilingi 500/= ya kuanzisha biashara ya kuuza matunda kwa
watu wanaojua umuhimu wa matunda.
Mtu anawezakuwa
na uwezo wa kukusanya faida ya shilingi 50,000/= (elfu hamsini) kama faida ya
siku moja, lakini asiwe na maendeleo yoyote. Donald J.Trump, na Robert T. Kiyosaki, katika kitabu chao
kinachojulikana kama “Why We Want You To Be Rich” katika masuala ya maendeleo kibiashara, walisema “Tatizo siyo kwamba tunaingiza shilingi
ngapi, bali tatizon ni, tunatunza shilingi ngapi? Lakini pia wote kwa
pamoja wanakubaliana kuwa, katika biashara, kwa waliowengi, “Tatizo siyo mtaji! Ila tatizo ni kukosa
elimu ya biashara na ujasiriamali” nukuu za waandishi hawa zinadhihirisha
ukweli kabisa kuwa, hata shilingi 1,000/= (elfu moja) ni mtaji tosha wa
kuanziasha baadhi ya biashara, ila shida kubwa ni kuifanya hiyo shilingi 1,000/=
izae na kuleta mtaji mkubwa zaidi.
#
ANGALIZO KWA MJASILIAMALI MDOGO (MUUZAJI WA MATUNDA)
Ø Kama una
mtaji mdogo, chonde chonde usifanye biashara ya kusafiri umbali mrefu, bali
fanya biashara ya kusafiri kwa umbali usiozidi lisaa limoja. Hii itakurahisishia
kuwa na uhakika wa kurudia bidhaa muda wowote utakapomaliza bidhaa, na hivyo
kufanya mzunguko wako kwenda haraka,
wenye tija na wenye kukupatia faida zaidi.
Ø Usikopeshe
zaidi ya nusu ya mtaji wako, maana kwa kufanya hivyo, unaweza ukajikuta unakosa
fedha ya kwenda kuchukulia mzigo, wakati ukiwa umeshauza mzigo wote (ila kwa
mkopo).
Ø Mkopeshe mteja
ambaye una uhakika wa kulipwa ndani ya masaa kadhaa, na siyo siku kadhaa.
Ø Uwe
mwaminifu na mkweli katika biashara zako
Ø Itetee
vyema biashara yako
Ø Ipende
biashara yako, kwa kuiona kama ndiyo kazi yako uliyoajiriwa.
Ø Uwe na
lugha nzuri kwa wateja wako! hata kama hutaki kumkopesha, si vyema ukamwambia
kuwa “sikopeshi” badala yake mwambie “kwa kweli leo sina hela ya kwenda
kuchukulia mzigo, mzigo huu ndio ninaoutegemea kuongezea mtaji wa leo”
mteja huwa ni mwelewa sana endapo kama utatumia lugha ya kumwelewesha kwa utaratibu
na bila kuharibu furaha yake aliyonayo siku hiyo.
Ø Kuwa na
bei rafiki na isiyomuumiza mteja (yaani unakuwa na watja wa kila aina, wapo
wale wenye uwezo mzuri, pia wapo ambao uwezo wao ni mdogo, ila kutokana na
sababu zilizo nje ya uwezo wao,inawabidi wapate bidhaa zao ili maisha yaende)
kwa mfano, kwa mjasiriamali anayeuza matunda, atakutana na wateja kama vile
wagonjwa, wajawazito na wamama waliojifungua siku si nyingi. Hawa wote
wanahitaji huduma ya matunda, hivyo ni vyema kwa muuzaji kujua saikolojia na
uwezo wa wateja wake.
Nakushukuru kwa
kufuatilia makala zangu katika blog yangu na katika kurasa zangu za mitandao
ya kijamii. Usikose kufuatilia makala zangu zingine, ni rahisi sana, ingia
kwenye blog yangu kisha bofya kitufe follow by e-mail. Mpaka
hapo utakuwa umefanikiwa kupata makala zangu mpya.
|
REJEA
Trump,
D.J & Kiyosaki, R.T (2006) Why We
Want You To Be Reach. Rich Press
Publishers.New York.
Shukran ndg yaani umefafanua kwa uzuri zaidi hadi mimi kichwa ngumu nimeelewa. Ahahahaaaa!!!! Ahsante sana
JibuFutaasante nawe kwa kusoma makala hii! naamini utakuwa umepata kitu kutoka katika makala hii.
FutaAise sijawai toa comment ktk blog leo umenishawishi vizuri broo
JibuFutandivyo ilivyo kka, kufanikiwa kibiashara, siyo jambo la kulala na ukaamka tajiri! bali inahitajika kujituma zaidi na kuheshimu mtaji ulionao.
FutaNimeukubali ushauri na nitaufanyia kazi
JibuFutavizuri! hatua moja ndiyo husababisha kutokea kwa hatua nyingine!
FutaDah, umenifumbua macho mwandishi, asante tukutane 2020
JibuFutaMungu atusaidie, ili 2020 iwe ni mwaka wa mafanikio
FutaNimeongeza kitu kikubwa sana asante sana
JibuFutaelimu ya biashara siyo hadi tufike chuo kikuu, bali ni kile unachokutananacho katika katika biashara unayoifanya na katika maisha kwa ujumla! KILA PESA NI MTAJI, kama mtu anatoka nyumbani na Tsh. 1000 anaenda mnadani kudaka mkanda mmoja, na kisha anautembeza na kuuuza Tsh 2000 hadi Tsh. 5000, hapo hajapata faida???
FutaNimeongeza kitu kikubwa sana asante sana
JibuFutaNatarajia kuanza bishara hii mwezi wa 3/2020. Najua changamoto zipo. Swali! Je utakuwa tayari kunisaidia kimawazo pind nahitaji ushauri? katika kuhoresha na katika changamoto pia.
JibuFutaBila shaka, nipo tayari tumia 0755482030
FutaAsnt kw ufafanuzi
JibuFutaBarikiwa san
Asante, nawe barikiwa pia kwa kupokea kipya ki mawazo
FutaAsanten sana. Mmenifanya nikafahamu kitu kwenye biashara. Naweza kupata group lenu la whatsap??
JibuFutaNaomba namba za whatsap?
JibuFutaNimekuelewa sana kaka umefafanua vizuri sana nimependa sana
JibuFutaasante kk kwa mrejesho mzuri
FutaShukrani mzee
JibuFutaNatamani kupata mawasiliano yako Moja kwa Moja mana nimeupenda mafundisho yako
JibuFuta