potofu kwani mtu yeyote anawezakuwa mjasiliamali endapo kama atatumia muda
wake, akiri yake na nguvu zake kujifunza zaidi juu ya wazo alilonalo au juu ya kazi, taaluma au biashara anayoifanya.
![]() |
Nyumba na gari za kifahari (Liabilities) |
Leo nitashiriki nanyi kuhusu tofauti ya Assets
na Liabilities.
Wajasiliamali tuliowengi bado hatujajua kutofautisha assets na Liabilities.
Robert Kiyosaki (1998) alitoa tofauti za maneno haya katika muktadha wa
![]() |
Kilimo (ni asset) |
Kiyosaki alisema kuwa, Assets ni kile kinachoingiza pesa mfukoni
mwako, na Liabilities
ni kile kinachotoa pesa kutoka mfukoni mwako.
Lakini pia kuna vitu vingine vinawezakuwa asset na pia vinawezakuwa Liability, hii inategemea na matumizi ya
mnunuzi wa kitu hicho. Kwa mfano, pikipiki ni asset endapo kama utaitumia katika shughuli za bodaboda. Itakuwa ni
asset kwasababu itakuwa inakuingizia pesa mfukoni mwako.
![]() |
Pikipiki (Ni asset, pia ni Liability) |
Kwa upande mwingine pikipiki inawezakuwa Liability endapo kama utaitumia kama nyenzo ya kupigia misele ili
kujitwalia sifa na ujiko mtaani na kuonekana kuwa una pesa.
Watanzania wengi tunakuwa masikini kwasababu tunapenda sana
kununua vitu ambavyo siyo assets, lakini katika mawazo yetu huwa tunavisema
kuwa ni assets. Kwa
mfano , utakuta mtu kanunua sofa, kwaajili ya kuweka ndani,
lakini wakati huo huo pesa anaipata kwa kufanya kazi ngumu! Yaani kashindwa
kuanzisha hata kibiashara
kidogo kikawa kinamuingizia pesa kwa urahisi na badala yake ananunua kitu cha starehe ili tu naye aonekane kuwa anapesa, wakati kiuhalisia hana pesa.
![]() |
Sofa (Liability) |
kidogo kikawa kinamuingizia pesa kwa urahisi na badala yake ananunua kitu cha starehe ili tu naye aonekane kuwa anapesa, wakati kiuhalisia hana pesa.
Pengine utakuta mtu kakopa pesa benki, wakati hata hana
malengo mahususi na pesa hizo, atakachokifanya ni kununua/kujenge jumba kubwa
tena la gharama na gari la kisasa la kutembelea ili aonekane kuwa ni mtu wa
kisasa,wakati hana hata biashara yoyote itakayomsaidia kurejesha mkopo huo
benki. Matokeo yake benki wanamfirisi na hatimaye anakimbia kujificha ili
aepuke aibu! Hayo ni mawazo mgando.
Swali
Kulingana na mtazamo wa Kiyosaki, mtu akinunua “Kiwanja” atakuwa amenunua asset? Au ni
Liability!