UTANGULIZI
Maana ya Semantiki
Richmond
(2012 anafafanua maana ya Semantiki
kwamba ni tawi la isimu ya lugha linalohusu viyambo vya Lugha.Anaendelea kusema
kuwa semantiki ni utanzu wa isimu unaojishuighurisha na maana ya maneno au
viyambo vya maneno katika Lugha . Swali
kuu katika wanasemantiki ni kuhusu nini
maana ya maana.Hata hivyo wanasemantiki hujikita katika kuchunguza maana katika viwango mbalimbali kama vile:
ngazi ya sayansi (fonimu), Neno, Virai,
Vishazi na hata sentesi. Anamalizia kwa kusema kuwa tawi hili la isimu limekuwa ni muhimu sana hasa kutokana na umuhimu wa mazungumzo kwani
ili mazungumzo yaelewekena ujumbe ufahamike panaitajika Maana.
King’ei
(2010), Semantiki, ni taaluma ya isimu inayofafanua maana katika lugha.
TUKI
(2004), Semantiki, ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchambuzi wa
lugha katika kiwango cha maana.
Kwa
ujumla tunaweza kusema kuwa Semantiki ni taaluma inayohusika na uchunguzi wa
maana katika lugha itumiwayo na mwanadamu.
Maana ya Pragmatiki
Masamba
(2004). Pragmatiki (Pragmatics), ni taaluma ya isimu inayojishughulisha na
uchunguzi na uchambuzi wa lugha katika mawasiliano. Lengo kuu la taaluma hii ni
kuchunguza namna lugha inavyotumiwa na wasemaji wake katika mazingira halisi,
kama kwa nini msemaji ameamua kusema hivi badala ya kusema vinginevyo,
anakabiliwa na masharti gani ya maamuzi?.
Leech
(1981), anasema semantiki inaangalia
maana ya matamshi, maumbo na Miundo katika lugha. Anaendelea kusema Maana ni sehemu ya umilisi na ufahamu wa
lugha, kujifunza Lugha ni kukubaliana na maana za vipengele vyote vilivyopo
katika lugha.
Richmond
(2012), anasema kwamba ni tawi la Lugha linalojihusisha na matumizi ya lugha
kwa kuzingatia Muktadha wa wazungumzaji husika. Hivyo Thomason anadai kuwa
pragmantiki inahusu zaidi mambo mawili: Matumizi na Muktadha.
Geoffery
(2012), anasema kuwa, dhana ya pragmantiki ilivumbuliwa katika miaka ya 1930 na
mwanafalfasa C.W. Morris na imeanza kujulikana kama Tawi tegmezi la isimu lugha
miaka ya 1970 ambapo kabla ya hapo pragmantiki ilihusishwa kama tawi la
kifalsafa, na kufafanuliwa kwa kuzingatia misingi mikuu miwili : Matumizi na
Muktadha.
Kwa
upande wake Yule (1996) anafafanua dhana ya pragmantiki kwa kusema kuwa ni
taaluma inayohusu mahusiano yaliyopo kati ya Maana ya lugha na watumiaji wa
mambo hayo.
Kwa
ujumla tunaweza kusema kuwa Pragmatiki ni taalumainayohusiana
na matumizi halisi ya lugha katika
muktadha tofauti na uelewa wake kama
vile malengo ya mzungumzaji na jinsi msikilizaji anavyopokea malengo
hayo,Mfano, matumizi ya lugha katika muktadha wa hotelini ambapo mtu anweza
kusema nipe chai tatu na akaeleweka
UHUSIANO KATI YA SEMANTIKI NA
PRAGMATIKI
A. Kufanana kati ya Semantiki na Pragmatiki
1.
Semantiki na Pragmatiki vyote kwa pamoja vinalenga kutoa ufafanuzi kuhusu
mchakato wa lugha na matumizi yake kulingana na muktadha wa wazungumzaji au
utumikaji wake kama sehemu ya mfumo wa mazungumzo sambamba, kufasili na
kufafanua mfumo tungamanifu wa mazungumzo katika lugha, na hili litafanikiwa tu
kwa kuzingatia maarifa ya lugha sambamba na ulimwengu halisi wa mazungumzo.
2.
Maana ya kisemantiki inaweza kuzalisha maana ya kipragmatiki, hii ina maana ya
kwamba maana inayopatikana katika
pragmatiki hutokana na semantiki. Mfano,
maana ya kipragmatiki ya neno mtoto kumaanisha mpenzi inatokana na maana ya
kisemantiki ambayo ni kiumbe kichanga amabcho kinahitaji matuzo na uangalifu
mkubwa katika malezi.
3.
Semantiki na Pragmatiki zote kwa pamoja zinahusiana, kwa maana kwamba
zinajihusisha na maana ya maana katika lugha. Wala haitokuwa sahihi kudhani
kwamba kufahamu tu maana ya viambajengo katika tungo, iwe neno, kirai, kishazi,
au hata sentensi kuwa ndio kufahamu kwa kile kilichokusudiwa bila kujali
muktadha ambao neno hilo limetumika.Mfano,
maana za maneno zinazopatikana katika muktadha mbalimbali kama vile sokoni,
shuleni na muktadha mwingine.
4.
Kuna baadhi ya dhana za kisemantiki hutegemea msaada wa maana za kipragmatiki
ili ziweze kufikisha ujumbe kwa baadhi ya hadhira pasipo kuharibu mazungumzo au
kumkwaza msikilizaji. Mfano, mtu
anaweza kumwambia mwingine kwenye umati wa watu kuwa funga mlango wako akiwa na
maana ya afunge zipu ya sehemu ya siri ili mtu huyo asijisikie vibaya au aibu.
5.
Vilevile matawi haya yotekwa pamoja hushughulikia maana kaika lugha. Pragmatiki
inashughulikia maana isiyo ya msingi bali maana inayotokana na muktadha,
husika.kwa mfanonenomtoto katika
muktadha wa kimapenzi ni msichana, wakati semantiki inashughulika na maana ya
msingi ambayo inatoa fasiri kulingana na kitu kinachoonekana.kwa mfanonenomtoto litafasiliwa kama ni
kiumbe kinacho zaliwa na binadamu ambacho kina umri chini ya miaka kumi na
nane.
6.
Matawi yote mawili hutumia dhana ya simiotiki ambapo hujaribu kuchunguza
uhusiano uliopo kati ya umbo na maana inayopatikana katika umbo hilo. Mfano, alama mbalimbali na matendo
halisi ambapo kuna kuwa na uhusiano kati ya maumbo hayo na maana zake.
7.
Semantiki na pragimatiki zote zinafanya kazi katika lugha yoyote ile siyo
Kiswahili peke yake yaani hazifungwi na mipaka ya lugha yoyote .Mfano; semantiki na pragimatiki
zinavyofanya za kuchunguza maana za maneno katika lugha mabalimbali kama vile
lugha za kibantu na lugha zingine.
B. Kutofautiana kati ya Semantiki na Pragmatiki
1.Kwa
mujibu wa Louise McNally(1993), katika makala yake ya Semantiki na Pragmatiki anasema kuwa, Katika pragmatiki maana
hutolewa huku ikihusishwa au kutegemeana na mzungumzaji wa lugha, hii inamaana
kuwa katika pragmatiki, maana ya neno au tungo inategemea nini mzungumzaji
anakusudia kusema. Mfano, mtu
anaweza kusema leo niko ovyo akiwa na maana ya kwamba hana hela WAKATI katika semantiki, maana hutolewa ikiwa safi na
hutolewa kama jinsi inavyopaswa kuwa kutoka katika lugha husika, na maana hiyo
ndiyo huchukuliwa kama ndiyo njia ya mawasiliano.Mfano, mtu ana kuwa wazi tu kusema kuwa leo sina hela.
2.
Neno katika semantiki ndilo hubeba maana ya msingi na hulenga maana halisi ya
neno kama jinsi ambavyo wazungumzaji wa lugha hiyo walivyolizoea toka enzi na
enzi. Maana hii ya msingi huwa haibadiliki katika jamii zote zinazotumia neno
hilo. Mfano, neno “baba” huwa na
maana moja tu ya msingi ambayo ni mzazi wa kiumeWAKATI katika pragmatiki, hali hiyo ni tofauti, ambapo neno
hutazamwa katika mtazamo wa kidhima huku likihusishwa na muktadha ambapo neno
hilo limetumika.Mfano, neno “mtoto”
hubadilika kulinga na muktadha ambapo kwa muktadha mwingine hutumika kama
mpenzi Hii ni kwa mujibu wa Carston (1998) na Louise McNally.
3.
Katika semantiki, maana hutegemea sheria sinazohusishwa na muundo wa sentensi
(sintaksia ya lugha) Hivyo muundo ndio unaoamua na kutoa matokeo ya maana
inayokusudiwa msikilizaji aipate. Mfano,
unga unaliwa na kuku. Hivyo endapo kama maneno hayo hayo yakiwekwa katika
mpangilio tofauti, pia hata maana yake hubadilika LAKINI katika pragmatiki, maana hufinyangwa kutoka katika mazingira
halisi ambayo neno husika limetumiwa na haifungwi na sheria za kimuundo. Mfano, mtu anaweza kusema unga unakula
kuku kwa sababu hakuna sharia inayomfunga.(Carston, 1998)
4.
Carston (1998) na Louise McNally, kwa wakati tofauti wanasema kuwa, tunapotumia
sentensi yenye maana tofauti na maana halisi basi aina hiyo ya maana tutaiita
kuwa ni maana ya mzungumzaji au maana kutokana na muktadha au maana ya matamshi
au pragmatiki. Hivyo kwa ujumla maana hiyo itakuwa ni maana ya mzungumzaji na
siyo maana ya jamii nzima.Mfano, mtu
anasema leo nimekauka wakati huo akiwa na maana ya kwamba leo sijakunywa pombe
ya aina yeyote ile hvyo hiyo itakuwa maana yake na sio ya jamii nzima WAKATI katika semantiki maana
inayopatikana katika sentensi, huwa ni maana halisi ambayo kila sehemu
huitambua na jamii za aina mbili au zaidi huweza kuwasiliana na kuelewana. Mfano, maana ya neno baba hutambulika
kama ni mzazi wa kiume kwa jamii zote.kwa kutumia maana hiyo, hivyo mzungumzaji
hujibiwa kama jinsi inavyopaswa kujibiwa kulingana na jinsi neno hilo
linavyosimama katika isimu ya lugha hiyo.
5.
Matawi haya mawili ya lugha, pia hutofautiana katika wigo wake (scope)
semantiki wigo wake ni mfinyu sana kwa sababu inajikita zaidi na kuchunguza
maana katika nakala tu, na kuchambua maana ya maneno na jinsi gani maneno hayo
yanaungana na kuunda sentensi iliyo na maana.Mfano, semantiki hujikita kuchunguza miundo sahihi ya sentensi kama
vile baba analima shamaba au kuku anakula unga, ni miundo ya sentensi ambayo
inaleta maana kamili WAKATI pragmatiki ina uwanja mpana sana kwani
inajishughulisha na maeneo mbalimbali zaidi hata ya kuchunguza nakala.Mfano, pragmatiki huchuichunguza namana
lugha inavyotumika katika maeneo mbalimbali,mfano katika eno la sokoni mtu
anaweza kusema mimi utumbo na akaeleweka. (Alghamdi, 2013)
6.
Katika semantiki, muktadha hutegemea zaidi sheria na taratibu za lugha. Hii ina
maana kuwa, lugha ndiyo huamua mzungumzaji atumie muktadha upi pindi
anapozungumza na hii huambatana na jinsi sheria za lugha zinavyohitaji WAKATI katika pragmatiki, maana ya
mzungumzaji hutegemea muktadha husika. Hii ina maana kuwa, muktadha ndio
hutawala lugha na kuamua ni tungo ipi itumike katika muktadha fulani, hata kama
inapingana na sheria za lugha hiyo (Alghamdi, 2013)
7.
Maana ya kipragmatiki kwa kiasi kikubwa huathiriwa na nia au kusudio au
saikolojia ya mzungumzaji na siyo kama jinsi ambavyo sentensi inavyomaanisha.Mfano, mtu anaweza kutumia neno ambapo
akawa na lengo la kuficha uma isijue nini kinaendelea kwani anaweza kusema
umekiona wapi kitabu changu leo wakati huo akiwa na maana ya mpenzi wake WAKATI katika semantiki, kusudio na nia
ya mzungumzaji ni sharti ikubaliane na kanuni za lugha husika, ikiwa ni pamoja
na kufuata taratibu za muundo wa sentensi yaani mpangilio wa viambajengo katika
sentensi.Mfano, mtu ana kuwa huru
kuongea kile ambacho anakimaanisha yaani kama ni kitabu basi anakuwa
anamaanisha kitabu kweli na sio vinginevyo (Carston, 1998)
8.
Recanati (2002), Jeffrey na Stanley (2003) wanasema kuwa, maana ya kisemantiki
haibadiliki badiliki kuendana na wakati (yaani wakati mwingine neno hutumiwa
kwa kurejelea maana iliyopita) hii ina maana kuwa semantiki inaweza kutupatia
maana ya tendo lililofanyika miaka mingi iliyopita.Mfano, neno hayati hurejea mtu ambaye tayari amekwishafariki na
hata kuzikwa pia WAKATI katika
pragmatiki, maana hubadilika badilika kuendana na wakati uliopo, na hivyo
kujikuta kuwa na utajiri wa maneno au tungo mbalimbali zenye kuelezea tukio
linaloendelea kwa wakati uliopo. Kwa
mfano, mtu anapokumbushwa kifo cha ndugu yake aliyefariki mwaka mmoja
uliopita, na kisha akaanza kutoa machozi. Hii inaonyesha aina mbili za maana
kisemantiki na kipragmatiki:
(a) Maana
inayopatikana kutoka katika taarifa kuhusu kifo, hiyo ni maana ya kisemantiki.
(b) Maana
inayopatikana kutoka katika tendo la
kutoa machozi, hiyo ndiyo maana ya kipragmatiki.
9.
Tafsiri inayopatikana katika semantiki ni maana maalumu inayotolewa katika
lugha WAKATI tafsiri inayopatikana
katika pragmatika ni tafsiri zaidi ya lugha, kwani huhusisha hata tafsiri ya
matendo mbali mbali ambayo mtu anayatenda. Mfano,
maswali yafuatayo yanaweza kuulizwa katika pragmatiki (i) Ni lini tendo hilo
limetendeka? Iwe ni kupitia lugha au njia nyingine yoyote (ii) Nini sababu ya
kufanyika kwa tendo hilo lililotendeka?. Kwa kutafuta majibu ya maswali hayo,
utakuwa unafanya tafsiri ya tendo lililotendeka, yaani tafsiri ya kipragmatiki
(Recanati, 2002)
10.
Kwa mujibu wa Chomsky kama jinsi alivyonukuliwa na Szabo (2005)anasema,
semantiki tunaweza kuiita kuwa ni langue yaani
umilisi wa lugha husika, yenye kuhusisha taratibu na kanuni zinazolinda lugha. Mfano, anavyotumia lugha kwa kufuata
kanuni au muundo ulio sahihi amabapo mtu huzungumza sentensi zenye mantiki kama
vile baba analima na mama anapika WAKATIpragmatiki tunaweza kuita kuwa ni
Paloe, yaani utendaji wa mtu binafsi katika kuitumia lugha
yake aliyokwisha kuwa na umilisi nayo.Mfano,
mtu anavyotumia lugha kadiri ya uwezo wake mfano, mtu anaweza kusema kuwa unga
unakula kuku. (Szabo, 2005)
11.
Semantiki ni taaluma inayohusika na uchunguzi wa maana katika lugha itumiwayo
na mwanadamu.Mfano, maana ya neno
mama ikiwa na maana ya mzazi wa kikeLAKINIPragmatiki
ni taalumainayohusiana na matumizi
halisi ya lugha katika muktadha tofauti
na uelewa wake kama vile malengo ya mzungumzaji na jinsi msikilizaji
anavyopokea malengo hayo,Mfano,
matumizi ya lugha katika muktadha wa hotelini ambapo mtu anweza kusema nipe chai tatu na akaeleweka.
12.
Semantiki imegawanyika katika matawi mawili yaani semantiki ya kileksika ambayo
hujihusisha na maana za maneno na mahusiano ya maana katika sentensi na tawi la
pili ni semantiki ya virai au sentensi ambayo hujihusisha na maana za maneno
katika kiwango cha kisintaksia WAKATI
HUO Pragmatiki hujidhihirisha katika mazingira mawili yaani maana
inayopatikana katika mazingira ya kiisimu. Mfano,
kuna baadhi ya maneno hayawezi kupata maana mpaka yatumike na maneno mengine
katika sentensi, maneno hayo kama vile na, juu ya kwa. Mfano, amekuja kwa basi.
Sura ya pili ni maana inayopatikana katika matumizi yake katika muktadha fulani
katika ulimwengu wa watumia lugha .Mfano, maana za maneno zitakazotumika katika
muktadha wa stendi, mfano mtu anaweza kusema nitafutie vichwa vitatu na
akaeleweka vizuri katika muktadha huo.
13.
Katika semantiki viwango vinavyochunguzwa ni pamoja na fonimu→mofu→maneno→virai
na sentensi ILI HALI Pragmatiki
huchunguza zaidi namna lugha ianvyotumika katika muktadha mbalimbali. Mfano,
muktadha wa buchani mtu anaweza kusema mimi
utumbo na akaeleweka vizuri kabisa.
Kama unahitaji huduma ya kuandikiwa makala katika tovuti yako, au huduma yoyote basi wasiliana nami kupitia:-
SIMU: +255 755 987 604, +255 789 198 345
E-MAIL: reubentanzania@gmail.com
HITIMISHO
Kwa
ujumla dhana hizi zinatumika sana katika ulimwengu wa watumia lugh na zinaleta
ugumu katika kuzitofautisha kwani zote hujikita kuchunguza maana za maneno
katika muktadha tofauti tofauti kama sehemu ya mfumo wa mazungumzo
sambamba na kufafanua mfumo fungamanifu wa mazungumzo katika lugha, na hili
litafanikiwa tu kwa kuzingatia maarifa ya lugha sambamba na ulimwengu halisi wa
Mazungumzo.
MAREJEO
Alghamdi,
R (2013)Similarities and Differences
between Semantics and Pragmatics.
Carston,R
(1998) The Semantics/Pragmatics
Distinction: a view from relevance theory. Katika UCL
Working Papers in Linguistics.
Geoffrey Finch (2012), Linguistic; Terms and Concepts. Palgrave. Macmillan publishers
Jeffrey,
C & Stanley,J (2003) Semantics,
Pragmatics, and The Role of Semantic content.Oxford University Press.UK
King’ei K. (2010). Misingi Ya Isimu Jamii, Taasisi Ya Taaluma Za
Kiswahili, Chuo Kikuu Dar-es-saalam.
Leech,
G (1981), Semantics, Harmondswoth:
Penguin books limited hazel, Watson & vinery Ltd.
Louise
McNally(1993),Semantics and Pragmatics,
katika WIREs Cognitive Science.University of Pompeu Fabra.
Masamba
D.P.B. (2004). Kamusi ya isimu na falsafa
ya lugha; Dare-es-Saalam.TUKI
Richmond
H Thomason (2012),What is semantics?
Second version:Oxford
UK
Recanati,F
(2002)Pragmatics and Semantics.Ibis
avenue de Lowendal.Paris France.
Szabo,
Z.G (2005) The Distinction between
Semantics and Pragmatics.Oxford University
Press.Oxford.
TUKI.
(2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu,
Oxford University press;TUKI,
Dar-es-Saalam.
Yule, G. (1996). Pragmatics, Oxford university press: Hong Kong.